2015-04-14 14:46:00

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 52 ya kuombea miito duniani, 2015


Kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya 52 Kuombea Miito Duniani, Baba Mtakatifu Francisko ametoa Ujumbe wake , ambamo anahimiza moyo wa kitume na Uenezaji Injili, iwe  kiini cha sifa na tabia yote ya wito wa Mkristo.  Kwa maneno hayo Papa ametoa mwaliko kwa vijana kutokuwa na woga katika kuufunua moyo wazi na kuyatolea maisha yao sadaka, hasa  kwa ajili ya kumtumikia mhitaji zaidi maskini , daima kwa mtazamo wa kujikatalia utajiri wa kidunia, katika utupu,  kumwendea aliye masikini zaidi.

Ujumbe wa Papa unaongozwa na jina:"Kutoka,Uzoefu msingi katika Miito". Ni maneno mazito yaliyochaguliwa na Papa Francisco kuongoza  Siku ya Kuombea Miito Duniani, ambayo itakuwa Jumapili ya tarehe 26 Aprili 2015, ikiwa ni adhimisho la 52 tangu kuanzishwa kwa Siku ya kuombea Miito Duniani.

Baba Mtakatifu Francisko  ameandika, katika Kanisa la Kitume “kimisionari” wito wa  Mkristo hauwezi kuzaliwa tu  ndani ya uzoefu wa utendaji wa kitume lakini hasa ni kwa mtu mwenyewe kujifunua  wazi katika ukweli , na kutoka katika yale aliyoyazoea  kwa ajili ya huduma kwa wengine, kwa mujibu wa  Biblia, kama ilivyokuwa kwa watu wa Mungu , walikubali kutoka katika  nchi waliyoizoea ili wapate kukombolewa kutoka utumwani, ni kutoka na  kupata maisha mapya katika Kristo. Kifungu hiki cha  maneno ya  Papa, kinazungumzia  historia nzima ya wokovu na ya mienendo ya imani ya Kikristo.


Papa anaeleza katika mzizi wa kila wito wa Mkristo, hutoka  katika yote mawili faraja na ugumu binafsi katika kuyaweka maisha kwa Yesu Kristo. Ni kutoka kunakodai  mtu mwenyewe kuyadharau ya maisha yenyewe na hisia zote za kibinadamu. Maelezo ya Papa pia yamefanya nukuu kwa Waraka wa Papa Mstaafu Benedikto XVI, "Deus Caritas Est" akisema  ni wito wa upendo, wenye  kuvutia na kuona zaidi ndani ya nafsi ya mtu mwenyewe, na  kuchochea kujifunua wazi na kujiunga katika safari ya maisha ya  kuelekea ukombozi  kwa njia ya kuitoa nafsi, katika huduma kwa wengine.

Nguvu hii ya kutoka - Papa anaandika - sio tu inalenga katika wito binafsi wa mtu, lakini katika utume wote wa kimisionari na uenezaji   injili kwa Kanisa zima, Kanisa lililo katika hatua ya kutoka, lenye uwezo wa kwenda kukutana na Wana wa Mungu katika hali zao halisi,  na kujali  mateso na  majeraha yao. Kanisa lenye kuinjilisha ameandika Papa , daima hukutana na watu , na kutangaza kwa uhuru kamili, neno la ukombozi wa Injili,  lenye kuponya kwa neema ya Mungu,  majeraha ya roho na miili, na  huwafufua maskini na wahitaji.  Wito wa Mkristo , huwasilisha  ahadi ya kweli, na huduma ya kujenga Ufalme wa Mungu duniani, ukioongozwa  kwa dhamira ya mshikamano, hasa katika  kuwaelekea maskini.

Kwa ajili ya Vijana zaidi , wito wa Papa unawatia shime , wasitiwe hofu na hali za wasiwasi na mashaka katika uhakika wa kutimiza ndoto za maisha ya kila siku, bali wanachotakiwa ni kuwa wazi katika kile wanacho tamani katika maisha yao. Ni lazima kwanza kutoka na  kuanza  kutembea katika nyayo za Yesu, kama alivyofanya Bikira Maria, mfano wa kila wito, ambaye hakuwa na hofu ya kusema 'Ndiyo’ kwa  wito wa Mungu.








All the contents on this site are copyrighted ©.