2015-04-13 15:21:00

Nyote mwaalikwa kutafakari kwa makini Huruma ya Mungu


 

Jumapili iliyopita, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,  Papa Francisko kwa mara nyingine alitoa mwaliko kwa watu wote duniani, kutafakari kwa makini fumbo la  Siku Kuu ya Pasaka , yenye kuonyesha kikamilifu Upendo wa kuokoa wa Mungu , uliojaa wingi wa rehema.   Papa alisema, kama ilivyokuwa kwa Mtume Thomas, nasi pia , katika Jumapili hii ya pili ya Pasaka , tunaalikwa kuyatafakari  makovu ya Kristo Mfufuka, ambaye ni huruma ya Mungu yenyewe, ambayo inapita mapungufu yote ya binadamu na kuangaza juu ya giza la uovu na dhambi.  Papa aliendelea kutaja kuwa ni  wakati  makini na  mrefu,  kwa ajili ya kupokea  utajiri mkubwa wa upendo na huruma ya Mungu, kama pia inavyotarajiwa iwe wakati wa adhimisho la Jubilee ya kipekee ya Huruma ya Mungu, aliyoitangaza kwa mara ingine, wakati wa sala ya masifu ya jioni siku ya Jumamosi, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la hapa Vatican . Papa aliizungumzia Huruma ya Mungu, kuwa ni  Yesu Kristo  mwenyewe, ambaye tunapaswa kumkazia macho yetu, kumtazama Yeye , Yeye ambaye daima anatutafuta , anatusubiri na anatusamehe, ni mwingi wa huruma  na wala hatiwi hofu na shida zetu. Katika majeraha yake,  hutuponya  na husamehe dhambi zetu zote.  Papa alieleza na kumwomba Mama Bikira Maria atusaidie pia sisi kuiishi huruma hii, kuhurumia wengine, kama Yesu alivyo na huruma kwetu.

Maelezo ya Papa yalijengwa  katika Injili ya Yohana, ambamo Mitume wa Yesu  walipokuwa wamekusanyika katika chumba  cha ghorofani ,Bwana aliwatokea mitume wake lakini Thomas hakuwepo.  Bwana alionyesha majeraha ya mwili wake  kwa wanafunzi wake, na kusema "Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma ninyi" (Yohana 20:21). Na hivyo aliwapa ujumbe wake mwenyewe, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, lakini usiku huo Thomas hakuwepo, na baadaye alipoelezwa kuwa wamemwona Bwana ,  hakutaka kuamini ushuhuda wa wengine. Alisema "nisipoona na kugusa majeraha yake - sitaamini" (Yohana 20:25). Siku nane baadaye -  Yesu anarudi kuwa katikati ya Wanafunzi wake na Thomas, akiwepo, alimtaka ayaguse majeraha ya mikono yake na ubavu wake.  Inakuwa kinyume na kutoamini kwake.  Papa anasema, kwa njia ya kuona ishara za mateso,  Thomas anaamini kikamilifu ufufuo wa Yesu.

Papa anamtaja Thomas  kuwa mfano wa wengi wasiotaka kuamini bila kuona wenyewe au kutenda wao binafsi. Baada ya upinzani wa awali na wasiwasi, hatimaye  anaamini ingawa mwanzo ilikuwa kwa  shida, lakini  sasa anaamini.  Na ndivyo Yesu anavyosubiri kwa uvumilivu na  katika sadaka ya mateso na dhuluma  kama  mgeni. Wengi wanataka kwanza kuziona ishara na kugusa majeraha yake. Lakini Yesu anasema,  "heri" walio amini bila kuona.  Mtume Thomas kwa kukutana na kugusa makovu ya Yesu anaamini, anayadhihirisha majeraha yake,  makovu  yake, kudhalilishwa kwake kwa  alama za misumari, kipimo thabiti cha maamuzi yake  kwamba alipendwa naye.  Thomas anajikuta mbele ya Masihi, mpole, mwenye huruma na mnyenyekevu.  Ndiye Bwana aliyekuwa akimtafuta  katika  kina  cha siri ya utu wake.

Na ndivyo ilivyo kwa wengi  wetu,  tunatafuta katika kina cha moyo,  kukutana na Yesu, kwa njia ya upole,  huruma na upendo, kwa utambuzi kwamba huko ndiko aliko.  Papa alieleza na kuhimiza kutafuta mawasiliano binafsi na Yesu kupitia wema na uvumilivu.  Thomas alipata maana ya kina ya Ufufuko wa Yesu, na kubadilishwa ndani mwake , kuitangaza  imani yake kikamilifu akisema, "Bwana wangu na Mungu wangu" (V. 28).

Baada ya maelezo hayo Papa alisalimia makundi mbalimbali ya waamini mahujaji waliofika Roma toka pande zote za dunia. Na pia alipeleka salaam zake kwa Makanisa ya Mashariki ambayo Jumapili yaliadhimisha Jumapili ya Kwanza ya Pasaka kwa Mujibu wa Kalenda yao. Na pia salamu za dhati kwa Waamini wa Armenia , waliofika Roma na kuhudhuria Misa wakisindikizwa na viongozi wao wa Kiroho, Ma patriaki na Maaskofu  wakionyesha upendo wake mkuu kwa Khalifa wa Mtume Petro , katika umoja wa Kristo.

Katika Jumapili hii, mara baada ya hotuba ya Papa  juu ya maadhimisho ya miaka mia ya kifo dini cha Waarmenia wengi,  Serikali ya Uturuki ilionyesha upinzani kwa kuufunga mara moja ubalozi wake katika Jimbo Takatifu, ikisema hawakubaliani na maelezo ya Papa Francisco.  Papa Francisco katika maelezo hayo alifanya nukuu ya  kawaida katika Hotuba ya Mtangulizi wake, Papa  Yohana Paulo II na Karekin II, maelezo waliyoyatoa mwaka 2001, ambamo walizungumzia mauaji ya Waarmenia, yaliyo anza mwaka 1915, kama "mauaji ya kimbari ya kwanza ya karne ya ishirini" wakati ambamo waliua Maaskofu, makuhani, kidini, wanawake, wanaume, watoto na hata wazee na wagonjwa  bila kujitetea. 








All the contents on this site are copyrighted ©.