2015-04-13 14:51:00

Kanisa liwe na ujasiri kusema wazi na ukweli


“Kanisa daima hutembea katika njia ya uwazi na ukweli, ni  kusema mambo kwa uhuru kamili”, ni maneno yaliyotolewa na Papa Francisko wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, Jumatatu hii mapema asubuhi.  Baba Mtakatifu  alieleza na kuongeza kama ilivyokuwa wakati wa Mitume baada ya ufufuo wa Yesu,  ni tu  Roho Mtakatifu,  mwenye kuwa na  uwezo wa kubadili mtazamo wetu,  maisha yetu, na ndiye  mwenye kuwapa wafuasi wa Yesu ujasiri wa kusimama imara katika njia ya uwazi na ukweli. Papa alisema waamini hawawezi kutangaza wazi yale wanayoyaona au kuyasikia, bila kuwa kuwa na Roho Mtakatifu. Papa alikazia kwa kurejea maneno ya Mitume Petro na Yohana, kama ilivyosomwa katika somo la kwanza “Ongeeni na kusema ukweli bila woga”.

Baba Mtakatifu alikumbuka jinsi Petro na Yohana, baada ya muujiza kuwatokea wakati wakiwa gerezani kwa vitisho vya Makuhani ili kamwe wasilitaje jina la Yesu, lakini wao, hawakuogopa, waliendelea  kumtkuza Munguna kulitangaza jina la Yesu kwa bidii , hata waliporejea tena kwa ndugu zao, walihamasisha zaidi na zaidi kulitangaza Neno la Mungu " kusema ukweli. " Na walimwomba  Bwana  azione hali halisi walizokuwa wakiziishi kwa wakati huo,  mateso  na vitisho dhidi yao , ili awajalie watumishi wake kubaki na ujasiri wote kutangaza neno lake Bwana. 

Papa amesema, hata leo hii, ujumbe wa Kanisa, unabaki kuwa  ni ujumbe wa njia ya uwazi, njia ya ujasiri wa kuutangaza ukweli wa Kristo.  Na kwa maneno haya mawili ya kawaida na mepesi kama Biblia inavyosema, waliweza mitume waliweza kupata ujasiri.   Papa alitoa ufafanuzi juu ya maeneo hayo akisema,  'ujasiri', 'uaminifu na uhuru maana yake ni , kusema wazi bila kuongopa  ... Ni maneno yenye kuwa na maana nyingi,ambayo hasa ni kuondokana na hofu  na kupita katika njia ya uwazi wa kusema mambo kwa uhuru kamili, bila woga..

Kisha Papa Francisco alirejea somo la Injili, ambamo Yesu anakutana na  Nikodemo,  juu ya kuzaliwa mara ya pili , juu ya "maisha mapya, tofauti na ya kwanza.  Katika hili Papa alisisitiza kwamba,  katika safari hii ya uwazi na shujaa wa kweli, ni tu  Roho Mtakatifu, mtendaji wa  kweli,  pekee mwenye kutupatia neema hii ya  kuwa na ushujaa wa kumtangaza Yesu Kristo. Papa Francisco ameutaja  ushujaa huo katika kuitangaza Injili, kuwa ndiyo wenye kutofautisha  kati ya Wakristo na kutangaza mambo ya kidunia kirahisi.  Wakristo wanapomtangaza Kristo si kama wanapiga porojo za kutafuta mashabiki  wengi zaidi kijamii, kwa kuwa wingi wa watu si hoja kwao. Lakini ujasiri wa Wakristo kumtangaza Yesu Kristo, unatoka kwa Roho Mtakatifu, anawatia moyo wa kuendelea kutangaza bila hofu.  

Papa aliendelea kufafanua maneno ya Yesu anapozungumzia kuzaliwa mara ya pili, akisema , hutufanya kuelewa  zaidi juu ya Roho Mtakatifu kwamba, ndiye mwenye kuleta  mabadiliko katika mioyo  yetu, na kwamba anakuja mahali popote, kama upepo, nasi tunaisikia sauti yake. Ni tu Roho  Mtakatifu mwenye  uwezo wa kubadili mtazamo wetu, na ndiye pekee mwenye kuleta mabadiliko katika historia ya maisha yetu.

Papa alikamilisha homilia yake  akiomba neema ya ujasiri kutoka kwa Roho Mtakatifu, akisema kuna njia nyingi  ambazo tunaweza kuchukua katika kuwa na ujasiri. Na Mama Kanisa baada ya Siku Kuu ya Pasaka, huwaandaa waamini wake  kumpokea Roho Mtakatifu.  Kwa ajili hii,  baada ya maadhimisho ya  fumbo la  kifo na ufufuo wa Yesu, tunaweza kukumbuka historia nzima ya wokovu" na "kuomba neema ya kupokea Roho Mtakatifu mwenye kutupatia  ujasiri  wa kweli  katika kumtangaza Yesu Kristo Mfufuka .








All the contents on this site are copyrighted ©.