2015-04-11 11:25:00

Askofu Jean de Dieu Raoelison ateuliwa kuwa Askofu wa Ambatondrazaka


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Antoine Scopelliti wa Jimbo Katoliki Ambatondrazaka, Madagascar kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401 § 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu msaidizi Jean de Dieu Raoelison kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka, Madagascar. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Raoelison alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Antananarivo.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.