2015-04-10 08:50:00

Kutangazwa kwa Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Huruma ya Mungu!


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kutangaza rasmi maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Huruma ya Mungu, kwenye Ibada ya Masifu ya jioni, tarehe 11 Aprili 2015 atawakabidhi pia wawakilishi wa Makanisa mahalia nakala ya Waraka wa maadhimisho ya mwaka wa Jubilee ya Huruma ya Mungu. Baba Mtakatifu anaadhimisha tukio hili katika mkesha wa Jumapili ya huruma ya Mungu iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Wakuu wa Makanisa makuu manne yaliyoko Jimbo kuu la Roma, watapokea Waraka huu ili uweze kusomwa rasmi Jumapili ya huruma ya Mungu.

Kardinali Marc Ouellet, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu, Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji wa Watu, Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, Askofu mkuu Savio Hon Tai-Fai, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, kama mwakilishi wa Kanisa kutoka Mashariki.

Kwa upande wa Kanisa Barani Afrika, Waraka huu utapokelewa kwa niaba ya SECAM na Askofu Barthelemy Adoukonou, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Monsinyo Khaled Ayad Bishay atayawakilisha Makanisa ya Kikoptik kutoka Alexandria pamoja na Makanisa mengine ya Mashariki.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.