2015-04-09 15:56:00

Jimbo kuu la Mwanza: Umuhimu wa maisha ya Sala na sakramenti za Kanisa


Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inaendelea kukuletea barua ya kichungaji iliyoandikwa na Askofu mkuu Thaddeus Ruwa'ichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania,  katika maadhimisho ya Mwaka Familia. Katika sehemu hii anazungumzia kuhusu maudhui kwa kukazia maisha ya sala, Sakramenti za Kanisa.

Hii ni kutokana na changamoto kubwa zinazoendelea kuikabili familia katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Familia zinapaswa kujikita katika maisha ya sala na kutoa kipaumbele cha pekee katika maisha ya sala. Wazazi na walezi wawafundishe watoto wao umuhimu wa sala sanjari na kuendeleza Ibada kwa Bikira Maria, ili kutafuta msaada na maombezi yake kama alivyofanya kwenye Harusi ya Kana.

Askofu mkuu Ruwa’ichi anawaalika waamini kuwa na uelewa mpana, kuadhimisha mafumbo haya kwa heshima; waamini wajitahidi kutubu na kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao. Waamini wahakikishe kwamba, wanatoa kipaumbele cha pekee katika maisha ya ndoa na familia mintarafu Mafundisho ya Kanisa. Waamini waondokane na uchumba sugu au “maisha ya suria”.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.