2015-04-08 14:41:00

Jimbo kuu la Mwanza: Familia katika Maandiko Matakatifu


Familia ya Mungu Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania, kunako mwaka 2014 limeadhimisha mwaka wa Familia. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda kukushirikisha utajiri unaojikita katika barua ya kichungaji iliyotolewa na Askofu mkuu  Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza katika maadhimisho ya Mwaka wa Familia. Barua hii iwasaidie waamini kujiandaa kikamilifu katika maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu familia itakayoadhimishwa mwezi Oktoba, 2015 hapa mjini Vatican.

Katika barua hii ya kichungaji, Askofu mkuu Ruwaichi anazungumzia kuhusu Familia katika Maandiko Matakatifu kwa kukazia masuala ya: kidini, kimaadili, kijamii na kitaalimungu. Anapembua kwa kina na mapana kuhusu maudhui, kazi na uwajibikabi sanjari na kusherehekea maisha. Leo, tunapenda kukushirikisha utangulizi unaobaianisha kwanini Jimbo kuu la Mwanza liliamua kuadhimisha Mwaka wa Familia, kunako mwaka 2014.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.