2015-04-05 13:05:00

Papa : unyenyekevu na heshima ni msingi wa maisha ya furaha kamili.


Kama ulivyo utamaduni wa Mapapa kwa Siku Kuu ya Pasaka , Papa Francisco majira ya adhuhuri , alitoa ujumbe wake kwa jiji la Roma na Dunia kwa ujumla , mbele ya umati mkubwa wa mahujaji na waamini waliofurika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Alisema , Yesu Kristo amefufuka! Upendo  umeshinda  chuki, uzima umekishinda kifo , mwanga umeipiga giza.  Yesu kwa upendo wake kwetu,  kwa hiari yake alivua utukufu wake wa Kimungu , na, akatwaa namna ya mtumwa akajinyenyekeza hata kifo, mauti ya msalaba. Kwa sababu hii Mungu amemtukuza na kumfanya Bwana wa ulimwengu. Yesu ni Bwana!

Ujumbe wa Baba Mtakatifu  unawahakikisha binadamu wote kwamba , kwa kifo na ufufuo wake, Yesu anaonyesha kwa kila binadamu njia ya maisha na furaha,  na njia hii ni kuwa mnyenyekevu na kukubali  hadi kudhalilishwa.  Maisha ya namna hiyo ndiyo huongoza  katika utukufu.  Ameonya ni tu wale ambao ni  wanyenyekevu wanaoweza kusonga mbele katika njia hii inayoelekea juu kwa Mungu (cf. Wakosai 3: 1-4). “Wenye kiburi hutazama chini kutoka juu na wanyenyekevu hutazama  juu  tokea  chini."

Baba Mtakatifu ameeleza na kurejea somo la Asubuhi ya Pasaka, ambamo  wanawake, waliwahimiza  Petro na Yohana kwenda mbio kutazama Kabuni, Nao walikuta li wazi na tupu. Walijongea lango la kaburi, wakainamisha vichwa vyao ili waingie kaburini. Papa amesema , hiyo ndiyo siri ya kuingia katika fumbo hili la wokovu , tunahitaji kuinamisha maisha yetu katika unyenyekevu, kusikiliza Neno la  Mungu na kuliishi kwa hiari. Ni kwa namna hiyo tu, mtu anaweza kuelewa utukufu wa Yesu na kuwa na  uwezo wa kumfuata katika Njia yake.

Papa alibaini , dunia inasema , ili kusonga mbele katika maisha ni lazima, kupania hivyo kwa gharama zote katika  hali ya ushindani.. Lakini Wakristo wanaamini , kwa neema ya Kristo, aliye kufa na kufufuka, ndiyo mbegu ya ubinadamu wote, unaotafutwa na  binadamu  katika kuhudumiana , mmoja kwa mwingine,  wala si  katika  kuwa kiburi, lakini badala yake ni katika kuheshimiana na utayari wa kusaidiana.

 Kuheshimu wengine haina maana ya kuwa dhaifu,  lakini nguvu ya kweli! Wale ambao kubeba yao Ndani ya nguvu za Mungu, upendo wake na haki yake, hawana haja ya kutumia  vurugu,  bali wao ni watu wa kuzungumza na kutenda kwa nguvu ya ukweli, fadhila na upendo.

Papa alieleza na kuomba kutoka kwa Bwana Mfufuka  neema ya kutoanguka katika majaribu ya majivuno na ufahali wenye  kuchochea  vurugu na vita, lakini katika  kuwa na ujasiri wa kusamehe kwa unyenyekevu na amani. Aliendelea kumwomba Yesu , Mshindi wa kifo, kupunguza mateso ya ndugu zetu Wakristo wanaoteseka  kwa  Jina lake, na wale wote ambao wanadhulumiwa kama inayojionyesha sasa katika migogoro na vurugu zinazoendelea kusikika duniani kote.  matokeo ya migogoro inayoendelea na vurugu.

Papa ameomba kwa ajili ya amani , na hasa kwa ajili mataifa yanayoteswa na vita na fujo  kama  Syria na Iraq, ili kwamba sauti ya silaha iweze  kunyamaza na ili mahusiano ya  amani, yarejeshwe  miongoni mwa makundi mbalimbali yanayoishi katika mataifa hayo pendwa . Na pia ameitaka jumuiya ya Kimataifa isijitenge mbali na majanga haya yaliyo nje ya ubinadamu,  yanayojitokeza katika nchi hizi na kusababisha watu kuishi katika hali duni  Ukimbizi.

Aidha Papa ameomba kwa  ajili ya amani kwa watu wote katika  Nchi Takatifu, ili waweze kukua katika utamaduni wa kukutana hasa kati ya Israel na Wapalestina , na ili  majadiliano na mchakato wa ya kurejesha amani , na mchakato wa amani kuwa tena, ili kukomesha miaka ya mateso na mgawanyiko.


Na pia kwa ajili ya  amani Libya, ambako kuna ujinga wa  umwagaji damu na vitendo vyote ushenzi na vurugu viweze  kusitishwa, na kwamba wote waweze kuishi kwa amani na mustakabali wa nchi, uweze kujengwa katika neema ya  kufanya kazi kwa maridhiano na ujenzi wa  ya udugu na mshikamano wenye kuheshimu utu wa mtu. Na ndivyo iwe kwa Yemen pia, ambapo wote wana hamu ya kuona  ukuaji wa amani, kwa manufaa ya watu wote.  Papa aleleza na kuweka tumaini lake katika huruma ya Bwana kwamba makubaliano yaliyofikiwa Lausanne, yaweze kuwa hatua mbele thabiti katika ujenzi wa usalama na udugu duniani.

Aidha Papa amehimiza maombi kwa Bwana Mfufuka kwa  ajili ya  zawadi ya amani  kwa mataifa kadhaa ya Afrika , yanayosumbuliwa na ghasia na fujo za umwagaji wa damu kama ilivyo nchini Nigeria, Sudan Kusini na maeneo mbalimbali ya Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Papa anaomba sala namaombi ya watu wenye mapenzi mema na ziweze kupekelewa na Bwana kwa ajili ya wote waliopoteza maisha ya.  Na kwa namna ya kipekee amewakumbuka vijana waliouawa Alhamisi iliyopita katika Chuo Kikuu cha Garissa Kenya , na wote waliotekwa nyara , au wale waliolazimishwa kuachana na makazi yao au wapendwa wao.

Papa pia hakuchelea kuomba mwanga wa Bwana Mfufuka , ulimulikie taifa la Ukraine, hasa kwa wale ambao wamevumilia vurugu na mgongano katika wa miezi ya karibuni. Ameliombea taifa hilo limeweze kugundua upya amani na matumaini kupitia uwajibikaji na dhamira ya vyama vyote.


Papa pia alitoa mwaliko wa kuombea  amani na uhuru kwa ajili ya wanaume na wanawake wengi , ambao sasa wameingizwa chini ya mfumo wa zamani na mpya ya utumwa  na  watu binafsi au  makundi ya uhalifu. Pia kwa ajili ya amani na  uhuru wa  waathirika wa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, ambao  mara nyingi wana ubia na mamlaka yanayotakiwa  kulinda amani na maelewano katika familia ya binadamu. Pia ni kuomba amani kwa dunia hii  inayokabiliwa na  wafanyabiashara wa silaha.

Mwisho Papa ,aliwakumbuka wote wanaohangaika kimaisha , akianza na wale waliotelekezwa  pembezoni na jamii, waliofungwa  jela, maskini na wahamiaji ambao ni hivyo mara nyingi hupambana na kukataliwa, wenye kudhulumiwa , wagonjwa na mateso mengine, watoto, hasa  waathirika wa unyanyasaji, ambao leo hii wamegubikwa katika huzuni  na  maombolezo, na wote na wanawake  kwa waume wenye mapenzi mema , waweze kusikia  na kufarijiwa na sauti ya Bwana Yesu akisema : "Amani kwenu" (Lk 0:36). "Msiogope, kwa maana Nimefufuka na daima nitakuwa Nanyi.
 

Baada ya kusoma ujumbe wake , Papa alisalimia kwa kutaja makundi mbalimbali ya mahujaji waliofika katika uwanja huu wa Mtakatifu Petro, tokea pande mbalimbali za dunia, na kwa wote walio kuwa wakimsikiliza kupitia njia za mawasiliano jamii. Kwao wote aliwapa Baraka zake za Kipapa za  Pasaka , akiwatakia kila lililo jema katika nyumba zao na wote wanaoishi nao au kukutana  na katika kuitangaza  furaha la Maisha Bwana Mfufuka , aliyeleta pamoja naye upendo, haki, heshima na msamaha.
alikamilisha na asante kwa uwepo wao, kwa ajili ya maombi yao na shauku yao katika  imani yako.
Na pia alitoa shukurani kwa Taasisi ya Uholanzi iliyopamba uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu  kwa ajili ya Siku Kuu ya Pasaka. 








All the contents on this site are copyrighted ©.