2015-04-04 08:45:00

Yesu anaendelea kuteseka hata leo


Hapa Vatican,   katika kipindi cha maadhimisho ya  Liturujia ya  Mateso ya Yesu ya Ijumaa Kuu ,  Padre Raniero  Cantalamessa,   Muhubiri Maarufu wa Vatican, majira ya Alasiri,  alihubiri katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, liturujia iliyofuatiwa na Ibada ya kuabudu Msalaba.


Padre Cantalamessa, aliangalisha katika sura ya Yesu inayoteseka mbele ya Pilato, iliyochorwa na Msanii wa Karne ya 16 , Jan Mostaert, ambayo inaonyesha Yesu  akiwa amevishwa taji la miiba kichwani, matone ya damu  yakitoka usoni kwake na kinywa chake kiko  nusu wazi, kama mtu mwenye  matatizo ya kupumua. Na juu ya mabega yake, kuna joho nzito chakavu, zaidi lilitegenezwa kwa chuma  kuliko nguo. Mabega yake yameshuka kutoka  kupigwa , na mikono yake  imefungwa pamoja kwa  kamba kwa  mara mbili. Licha ya hayo , Yesu ameshika fimbo ya mwanzi katika mkono wake na mwingine mfuko wa  matawi katika nyingine, alama mzaha zilizo fanywa na watesi  wake. Yesu  hakuweza kutikisa hata kidole chake , hadhi yake ikiwa imefutwa kabisa na kuwa mtu asiyekuwa na uwezo wowote katika jamii,  na hivyo anakuwa ni mfano halisi wa historia ya  watu wateswa wa nyakati zote. 

Padre Cantalamessa ametafakari  mateso ya Yesu , kama mwanafalsafa Blaise Pascal alivyo andika "Kristo atakuwa katika uchungu mpaka mwisho wa dunia; hivyo hatupaswi kusinzia nyakati zote.. Maneno ya mwanafalsafa huyo, yana maana kubwa katika fumbo la mateso ya mwili wa Kristo, kwa kuwa wafuasi wake wanaendelea kuyaishi mateso hayo.  Yesu yuko katika uchungu mkubwa mpaka mwisho wa dunia kwa ajili ya kila mtu iwe mwanamke  au mwanamme. Na si tu kwa ajili ya waumini ndani ya kanisa lakini kwa wote wenye kukabiliwa matatizo na mahangaiko kama ya uhaba wa chakula, maskini wasiokuwa na kitu, waliofugwa gerezani kwa dhuluma , wagonjwa na dhiki zingine

Katika kutafakari mateso hayo, Padre Cantalamessa ametahadharisha, kuepuka kujumuiya hali ngumu na matatizo ya kijamii,  njaa, umaskini, ukosefu wa haki, unyonyaji na  udhaifu, akisema, kwani imekuwa ikifanyika hivyo siku zote ,  huzungumzwa  kwa namna hiyo kila mara  (na  kamwe hakuna jibu la  kutosha.),badala yake hujenga  hatari za kuchukuliwa kama ni mambo ya kawaida ya wote  badala ya kumlenga mtu mwenyewe mhusika. Padre  Rainero ,alipendekeza  mateso , yatazamwe katika mtazamo wa kila mtu binafsi. Kutazama tatizo kwa kila mtu , akitambuliwa kwa jina, iwe kwa matatizo yake yanayofanywa kisirisiri au yale yanayoonekana wazi, hali ngumu na hasa mateso yanayosababishwa na binadamu dhidi ya binadamu wengine , wakiwemo hata watoto .

Padre Cantalamensa ameendelea kuyatafakari matukio haya ya mateso kwa nyakati hizi zetu, akisema leo hii kuna  wafungwa wengi  wanaojikuta katika hali hiyo kama  ya Yesu ndani ya ukumbi wa Pilato: peke yao, mkono yao ikiwa imefungwa , wenye kuteswa bila huruma na maaskari, au wale wanaoteseka  kisaikolojia  kwa ukatili wa wale wanaofurahia kuwaona wakiteseka. “ Hatupaswi kuwaacha peke yao watu hao ! "

Muhubiri ameendelea kusema, neno lililotumika Tazameni  "Ecce homo!" linatumika si tu kwa waathirika lakini pia kwa watesaji, maana yake  "Tazama kile mtu anaweza kufanya!" Nasi  pia , kwa hofu na kutetemeka, hebu pia kusema, "Tazama kile binadamu anaweza kufanya!" Ni kwa umbali gani , tupo katika mwendo huu wa kusonga mbele na mabadiliko ya binadamu katika mwanga wa kisasa katika ubinadamu.

Padre Cantalamessa ameeleza na kusema , ni wazi si Wakristo peke yao wanao kiishi kipindi cha mauaji na ghasia  zinazoendelea kufanyika duniani lakini pia hatuwezi kupuuzia ukweli kwamba katika mataifa mengi Wakristo wamekuwa walengwa. Yesu aliwaambia wafuasi wake , saa yaja,atakapodhania kila auae ya kuwa anamtolea Mungu Ibada( Yn 16.2, 3) Na  hayo watayatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala Mimi.  Pengine maneno hayo ya Yesu kwa sasa yanatimia zaidi kuliko hata ilivyokuwa siku za nyuma. Na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa Wakristo wengi katika Pasaka ya mwaka huu.








All the contents on this site are copyrighted ©.