Kama kawaida ya kila Jumatano, majira ya asubuhi, Baba Mtakatifu alitoa katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro . Katika katekesi hii alianza kwa kuitaja Alhamisi Kuu ambamo ,kwa Ibada ya Karamu ya Mwisho ya Bwana , hukifungua kipindi cha Siku Tatu Kuu tatu kuelekea adhimisho la Fumbo la Pasaka, “Triduo Pasquale “ ambamo mna mateso, kifo na ufufuko wa Bwana, ikiwa ni kilele cha mwaka mzima wa Liturujia na pia hatima ya maisha yetu ya Kikristo.
Alisema , Siku Kuu hizi Tatu , huzinduliwa na maadhimisho ya karamu ya mwisho ya
Bwana. Yesu katika usiku wa mateso yake, aliutoa mwili wake kwa Baba, mwili wake na
damu yake kupitia alama za chakula , Mkate na mvinyo , akiwalisha Mitume wake na kuwataka
waendeleze hili kwa ukumbusho wake. Papa ameendelea kuzungumzia Injili inayosomwa
katika tukio hili la Alhamisi Kuu, akikumbuka jinsi Yesu alivyoosha miguu wanafunzi
wake, ishara ya huduma, fadhila na unyenyekevu. Na alitaja pia maana ya tukio hilo
katika mtazamo wa Yesu katika Ekaristi.. Alifafanua , Yesu anawaosha miguu mitume
wake kama mtumishi. Aliiosha miguu ya Petro na wanafunzi wake wengine kumi na moja
wanafunzi (cf. Jn 13.4-5). Kwa ishara hii ya kinabii, anaonyesha hisia ya maisha yake
na mateso yake, kwamba ni huduma kwa Mungu na kwa wengine:akiyatimiza maneno yake
mwenyewe, "Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumika" (Marko 10:45).
Hii pia inaonyesha kilichotokea katika ubatizo wetu, wakati neema ya Mungu, inatutakasa dhambi na sisi kujiweka kwa Kristo (Kol 3:10). Na ndivyo inavyotokea kila wakati waamini wanapofanya kumbukumbu ya Bwana katika Ekaristi: inakuwa ushariki na Kristo Mtumishi, kwa kutii amri yake ya upendo, kupendana kama Yeye alivyotupenda (cf. Jn 13:34; 15:12). Lakini Papa ameonya katika umoja huu Mtakatifu, ni lazima kuwa na utambuzi wa dhati, katika utayari wa kuhudumiana mmoja kwa mwingine ili tuweze kuutambua Mwili wa Bwana. Yesu aliutoa sadaka mwili wake kikamilifu katika huduma.
Kisha Papa alizungumzia pia Liturujia ya Ijumaa Kuu ambamo waamini wanatafakari Fumbo la mateso na Kifo cha Kristo na kuabudu Msalaba . Amesema kwa kuyatoa maisha yake sadaka msalabani , dhambi zetu zote zinaondolewa kupitia upendo wake , upendo kamili tunaotakiwa kuuishi na kuueneza.. Katika dakika za mwisho za maisha yake , kabla ya kukabidhi roho kwa Baba, Yesu alisema: yametimia (Yohana 19:30). Papa amefafanua zaidi kwamba, Neno hili imetimia lina maana kwamba Yesu, kazi ya wokovu imetimia, kwamba maandiko yanatimilika katika upendo wa Kristo, Mwana kondoo anayeuawa. Yesu, kwa sadaka yake ya maisha , alifanya mageuzi katika ukosefu wa usawa, kwa upendo mkuu.. Upendo huu umekuwa ukishuhudiwa kwa karne na karne na wanaume na wanawake, kwa ushuhuda wa maisha yao, yenye kutoa miali ya tafakari juu ya upendo kamili, upendo kamili usiokuwa na doa.
Papa alieleza hilo na kutoa mfano wa ushahidi wa kishujaa wa wakati wetu, wa Padre Andrea Santoro, Padre wa Jimbo la Roma na Mmisionari ,aliyeuwa Uturuki, ambaye siku chache kabla kuuawa huko Trabzon, aliandika hivi: "Mimi naishi hapa kati ya watu hawa, nikimruhusu Yesu afanye hivyo kupitia kwangu . Yesu aliweza tu kuleta wokovu, kwa kutoa mwili wake mwenyewe sadaka, Na ndivyo ili kuyashinda. maovu ya dunia, ni lazima machafu na maumivu yote kwa pamoja, yamwilishwe katika nyama yao wenyewe njia, kama Yesu alivyofanya "
Papa aliomba mfano wa imani ya mtu huyu wa nyakati zetu, na wengine wengi, viweze kutusaidia katika kutoa sadaka ya maisha yetu kama zawadi ya upendo kwa ndugu, tukimwiga Yesu Mwenyewe
Papa alikamilisha mafundisho yake na tafakari juu ya Jumamosi Kuu ambamo kwanza tunauona mwili wa Yesu ukiwa umelala kaburini , wakati wa giza nene la usiku, linaloonekana wakati mwingine kutaka kupenya katika nafsi zetu ,na kukatisha tamaa nguvu ya upendo, ikififishwa na giza. Lakini giza hili, linashindwa taa na moto wa upendo wa Kristo, wenye kugeuza mawe ya maumivu na mateso , na kuwa nafasi ya matumaini. Hapa ndipo kuna siri kubwa ya Pasaka!
Katika usiku huu Mtakatifu, Kanisa linapata kumulikiwa na mwanga wa Mfufuka. Na likiwa Maria, Kanisa linakesha macho kwa mwanga wa imani, na katika kila tumaini. Papa alieleza na kusisitiza kwamba , katika siku hizi tatu si tu kufanya maadhimisho ya kumbukumbu lakini ni wakati wa kuzamisha mioyo yetu ndani ya fumbo hili la wokovu , tukikiishi kipindi hiki na hisia za kweli za uwepo wa Kristo ndani mwetu. Kwa namna hiyo ndivyo tunaweza kupokea baraka za Pasaka.
All the contents on this site are copyrighted ©. |