Uteuzi :
Baba Mtakatifu Francisko amemteua kuwa Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Elimu Katoliki , Muadhama Kardinali Joseph Versaldi, ambaye hadi uteuzi huu mpya ni Rais wa Idara ya Uchumi katika Jimbo Takatifu.
Aidha Baba Mtakatifu ameteua Maaskofu wasaidizi wawili kwa ajili ya Jimbo Kuu la Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Padre Donatien Bafuidinsoni, SI, ambaye kwa wakati ni Wakili katika Mahakama ya Jimbo Kuu , na pia Mons Jean-Pierre Kwambamba Masi, ambaye kwa wakati huu ni mmoja wa Maafisa katika Shirika kwa ajili ya Ibada na Nidhamu ya Sakramenti.
Askofu Mteule Bafuidinsoni, ametajwa kuwa Askofu wa Jina wa Gemelle di Bizacena na Askofu Mteule Kwambamba Masi, kuwa Askofu wa Jina wa Naratcata.
Pia Papa amemteua kwa Mjumbe katika Utawala wa urithi katika Kiti Kitakatifu , Muadhama Kardinali Rainer Woelki, Askofu Mkuu wa Cologne (Ujerumani).
All the contents on this site are copyrighted ©. |