2015-03-28 16:25:00

Masikitiko ya Papa Francisko kwa waathirika wa mafuriko Chile na Perù


Hivi karibuni Chile na Perù zimekumbwa na mafuriko makubwa kiasi cha kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao pamoja na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu. Baba Mtakatifu Francisko Ameguswa sana na hali hii kiasi cha kutuma ujumbe wa upendo na mshikamano wa dhati kwa waathirika wa mafuriko haya nchini Chile na Perù.

Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, anawataka Mabalozi wa Vatican katika nchi hizi kufikisha ujumbe wa mshikamano kutoka kwa Baba Mtakatifu kwa waathirika wa mafuriko haya. Ni matumaini yake kwamba, Jumuiya ya Kimataifa na watu wote wenye mapenzi mema wa taonesha mshikamano wa dhati kwa kuwasaidia waathirika ili kuonja upendo na mshikamano wa Kikristo, ili watu hawa waweze kuanza tena safari ya maisha yao kwa matumaini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.