2015-03-28 10:04:00

Askofu mwandamizi Anagbe ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Makurdi


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uamuzi wa kung’atuka kutoka madarakani uliowasilishwa kwake na Askofu Athanasius Atule Usuh wa Jimbo Katoliki Makurdi, Nigeria kadiri ya sheria za Kanisa namba 401 Ibara ya 2. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu mwandamizi Wilfred Chikpa Anagbe wa Jimbo Katoliki Makurdi kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Makurdi. Askofu mteule kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Askofu mwanadamizi wa Jimbo Katoliki la Makurdi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.