2015-03-27 14:04:00

Usugu wa TB bado kitisho kwa afya ya umma.


Ripoti ya Wanasayansi iliyotolewa katika  jarida la habari za tiba la London,  inataja ongezeko la  vijidudu sugu vinavyosababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kwa dawa zinazotumika kupambana na wadudu hao, ni tishio kali kwa afya ya umma.  Ripoti ya Wanasayansi  inabaini kwamba,  katika kipindi cha miaka  35 ijayo   usugu wa wadudu hao, kwa dawa nyingi zinazotumika, utaua wastani wa watu milioni 75 na inaweza kugharamu kiasi cha dola trilioni 16.7  katika uchumi wa  dunia, ikiwa ni sawa na pato la mwaka mmoja la Umoja wa Ulaya.

Kutokana na ripoti hiyo, kikundi cha Wabunge Uingereza , siku ya Jumanne walionyesha kujali  taarifa hiyo na kutoa wito kwa serikali zichukue hatua   makini zaidi tangu sasa, kupambana na usugu  huo, ili madhara zaidi yasitokee, si tu   kwa uhai wa watu tu lakini pia kwa uchumi wa  dunia ,unaotishiwa kudidimizwa kwa  asilimia 0.63 kwa mwaka .

Ripoti inaendelea kubaini kwamba , vifo , uharibifu wa kiuchumi na athari za majanga,  vimesababisha vifo kwa watu milioni 42 kwa mwaka, tangu mwaka 1980. Na kwamba zaidi ya silimia 90 ya jumla ya maisha yaliyopotea katika kipindi cha miaka 1980 hadi 2012, ilitokea katika nchi zenye kipato kidogo , ikionyesha  kuwa kipingamizi kizito katika shughuli zake za maendeleo. Hili limeelezwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kupunguza hatari za majanga duniani (UNISDR). Na hivyo takwimu hizi zinaonyesha haja ya kidharura ya dunia kuwa na ushirikiano wa karibu katika kupambana na maradhi ya kifua kikuu.

UNISDR inasema ni kupoteza muda kuwa na uwekezaji mkubwa katika mambo mengine, na  kupuuza  matatizo mengine yanayosababisha umaskini  kupitia mifumo ya mipango mibovu ya makazi ya watu, majibiladia,  miundo mbinu katika afya na elimu.

Ofisi imeonya kwa kuzingatia kwamba imepita sasa miaka kumi tangu serikali zilipoweka sahihi mpango wa kidunia wa kupambana na Kifua Kikuu juhudi zinazojulikana Kama Mtandao wa Utendaji wa Hyogo,bado hakuna mafanikio ya kuonekana katika kupunguza  hatari za ugonjwa huo. 

Shirika la Afya la Dunia mwaka jana lilitaarifu kwamba dawa za kuzuia Kifua kikuu zinaonyesha kutofanya kazi vizuri kutokana na uwepo wa kesi nyingi mpya za ugonjwa huo katika kiwango cha ambukizo la watu 480,000, za mwaka 2014. 

Imehaririwa na T.J Mhella 








All the contents on this site are copyrighted ©.