2015-03-26 12:06:00

Njaa kali yanyemelea Kenya


Kwa mujibu wa habari iliyo chapishwa na AllAfrica, baadhi ya maeneo yaliyo kosa mvua za kutosha  katika kipindi cha msimu wa  kustawisha mazao , inakadiriwa watu wapatao  milioni 1.6, wanaweza kukabiliwa na njaa kali nchini Kenya . Hilo lilielezwa katika mkutano ulio kutanisha wabia mbalimbali kwa ajili ya kutathmini kwa pamoja, msaada utakao hitajika kusaidia watu katika kipindi cha miezi sita ijayo , wanaoishi katika maeneo yaliyoathirika na ukame.  Matokeo ya tathmini , yalionyesha watu wapatao milioni 1.6, watahitaji  chakula cha msaada hasa wanaoishi Mandera, Garissa, Isiolo, Wajir na maeneo ya Mto Tana. Mikoa mingine iliyoathirika ni Tharaka Nithi, eneo la Meru, Makueni na Kitui. Ukame huu pia unaathiri mifugo katika  maeneo hayo. 








All the contents on this site are copyrighted ©.