2015-03-25 15:08:00

Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na chumi wa Afrika Jumatatu ijayo


 (Addis Ababa ) Katika Makao Makuu ya Tume ya Umoja wa Mataifa Kitengo cha Uchumi  Afrika (ECA) Jumatatu ijayo 30 Machi,  kutafanyika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi,  unaotanguliwa na vikao vya watalaam katika uwanja huo, walioteuliwa na Umoja wa Afrika kama washauri katika masuala ya fedha na uchumi , mipango  na ushirikiano. Aidha kutazinduliwa Ripoti ya Uchumi juu wa Afrika , chini ya jina Viwanda kupitia Biashara. Na pia ratiba inaonyesha itakuwa ni kuanza kwa warsha iliyoandaliwa na mtandao wa dunia nzima na  pia matazamio ya kupata ahueni katika kufufua uchumi wa mataifa yaliyokumbwa vibaya na ugonjwa wa ebola .Ni majadiliano ya wiki nzima , kwa ajili ya kuona mambo yanayostahili kupata kipaumbele kwa ajili ya maendeleo ya Afrika .

Mada Kuu ya  mikutano ni “Utekelezaji Agenda  ya 2063 - Mipango, Uhamasisha na Fedha kwa ajili ya Maendeleo”. Mkakati  wa Agenda 2063 uliandaliwa kwa ajili ya kutengeneza malengo ya maendeleo ya Afrika , kama ilivyopitishwa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika, mwaka jana  kwa madhumuni ya kuongeza matumizi  safi ya rasilimali za Afrika  na kuhakikisha  mabadiliko chanya katika uchumi  ndani ya miaka 50 ijayo.

Mwandishi Janet Mhella








All the contents on this site are copyrighted ©.