Kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano muhimu wa Kimataifa utakaofanyika Addis Ababa , mwezi Julai 2015, juu ya utekelezaji wa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) , watalaam wa uchumi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa , hivi karibuni walikutana mjini Geneva ,mazungumzo yaliyo fadhiliwa na Tume ya Uchumi kwa Ulaya . Mkutano huo ulijadili utekelezaji wa malengo ya maendeleo kama changamoto kubwa katika upatikanaji wa matrilioni ya dola kwa kila mwaka.
Amina Mohammed, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,ambaye pia ni Mwakilishi
Maalum katika Mipango ya Maendeleo ya baada ya Malengo ya mwaka 2015, alizungumza
katika mkutano huo, kwa kutoa wito kwa mataifa kwamba, umefika wakati kwa serikali
kuwajibika zaidi na hatua za utekelezaji kwa ahadi walizotoa.
Mwandishi wa habari hii Daniel Johnson, anaendelea kumnukuu Bibi Amina Mohammed,
kwamba kwa hitaji la kiwango cha trilioni kati ya $ 5 hadi wa $ 7 kwa mwaka, kwa
ajili ya miradi ya miundombinu peke yake ni muhimu kuwa na mikakati tangu sasa, katika
jinsi ya kupata fedha hizo. Na kwamba , changamoto kama vile kutokomeza umaskini
ifikapo mwaka 2030 na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, yana mwelekeo wa
kugharimu fedha nyingi zaidi na hasa iwapo mataifa hayatajipanga vyema, katika
kutimiza ahadi zake za kifedha.
Amina Mohammed, aliendelea kusema kwamba kuna kila aina ya majawabu yaliyowasilisha
mezani kimsingi yakionyesha mazingira ya uwepo wa nyenzo za kupata fedha, tena si
tu mabilioni, lakini matrilioni ya fedha zinazohitajika. Lakini fedha hizo zitapatikana
iwapo serikali zitawajibika katika kushika usukani wa kufanikisha malengo 17 ya Umoja
wa Mataifa, yanayo waniwa na wote. Bi Mohammed kati ya changamoto nyingi zilizowasilishwa
mezani, ametaja haja ya kukomesha ukwepaji wa kodi na mtiririko wa fedha haramu.
Aidha alitaja utayari wa sekta binafsi kushirikiana katika utafuta wa matrilioni ya
dola zinazo hitajika, lakini sekta hiyo imefungwa na baadhi ya vipengere vinavyo hitaji
kulegezwa.
Matokeo ya mkutano Geneva yatatumika katika mkutano muhimu wa kutafuta ufadhili katika mipango ya maendeleo, utakao fanyika Addis Ababa mwezi Julai 2015.
All the contents on this site are copyrighted ©. |