2015-03-03 15:58:58

Papa ashukuru ujasiri wa makanisa Afrika ya Kaskazini: Asante kwa ujasiri wenu"


Baba Mtakatifu Francisko ametoa shukurani zake za dhati kwa Kanisa nchini Libya na jumuiya yote ya Kanisa katika eneo la Afrika Kaskazini kwa ujasiri wake na amani inayoendelea kuwepo licha ya kuwepo milipuko ya matukio ya ghasia za kudai uhuru na hadhi zaidi. Papa alitoa shukurani hizo wakati akizungumza na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Afrika Kaskazini , CERNA, ambao wako katika hija yao ya kitume katika Kiti Kitakatifu wiki hii. CERNA huunganisha pamoja Maaskofu kutoka Morocco, Algeria, Tunisia na Libya.


Katika hotuba yake Papa ametaja Maaskofu hao kuwa katika ukingo wa dunia na ni uso na moyo ambako Mungu huweza kuwafikia watu wa eneo hilo. Papa kwa moyo wa upendo na kibaba aliwazungumzia kwa makini, viongozi wa Kanisa wa eneo hilo ambao wako tayari hata kuhatarisha maisha, kwa ajili ya kuliongoza na kulinda kundi la dogo la Kanisa katika eneo ambapo sauti ya kengele ya kanisa hunyamazishwa na utamaduni mahalia.

Papa alionyesha kutambua jinsi Afrika Kaskazini kwa miaka mingi, imekuwa nchi ya ushindi wa uhuru mkubwa wa dhamiri" na "utu" na kwa pamoja, imekuwa ni kambi ya vita vya silaha kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa hili, Papa alitoa shukurani zake za dhati kwanza kwa Maaskofu , miongoni mwa wengi wanaostahili kupewa sifa , na hasa kwa Kanisa nchini Libya kwa ujasiri, uaminifu na uvumilivu ulioonyeshwa na viongozi wake wa Kanisa, Watawa na walei, na hasa kubaki katika nafasi zao licha ya hatari nyingi zinazo wakabili. Papa amewataja kuwa ni Mashahidi wa kweli wa Injili. Hivyo aliwashukuru na kuwahimiza kwa moyo wote, waendelea na juhudi zao, kuchangia amani na maridhiano kwa kanda nzima ya Afrika Kaskazini.

Papa Francisko amesisitiza umuhimu wa kujiunga katika mazungumzo ya muda mrefu kwa ajili ya kujenga amani hasa mahali penye kuwa na uharibifu. . Alikumbusha kwamba ubunifu wenye upendo, una uwezo wa kufungua fursa nyingi zenye kuingiza pumzi ya Injili katika utamaduni na katika mazingira mbalimbali ya kijamii. Ni dawa nzuri katika kupambana na aina yoyote ya ghasia na hasa kupitia mipango ya elimu, ugunduzi na kukubali tofauti kama utajiri na ustawi wa jamii. Papa aliendelea kuwaonyesha Maaskofu, umuhimu wa Mapadri na watawa katika majimbo yao , kushiriki katika mafunzo ya kiekumeni na majadiliano kati ya dini. Aidha Papa aliitumia nafasi hii kutoa pongezi kwa kutumia miaka 50 ya Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya masomo ya Kiarabu na masomo ya kiislamu (PISAI) iliyoanzishwa Tunis, na kukumbuka vyema kazi nzuri za kiekumeni zinazofanyika katika taasisi ya Mowafaqa yenye kuwa na makao yake makuu Morocco .

Papa alitaja silaha nyingine ya Kanisa licha ya kukutana na mazungumzo kwamba ni matendo ya huruma kwa kila binadamu bila ubaguzi. Na aliwashukuru Maaskofu wa Afrika Kaskazini kwakuwa wamekuwa wakiliishi hili mara nyingi kwa njia ya unyenyekevu, wenye kuonyesha upendo wa Kristo na Kanisa kwa watu maskini, wagonjwa, wazee, wanawake hata wafungwa", pamoja na wahamiaji wengi wa Afrika wanaotafuta kuhama nchi zao kwa ajili ya kwenda kutafuta malisho mazuri zaidi sehemu zingine . Hata katika "kutambua utu wa ubinadamu wao na kufanya kazi kwa dhamiri ya ubinadamu katika uso wa wenye kuonyesha kwamba Mungu anampenda kwa kila mmoja wao.
Papa hakuishia hapo lakini pia aliwatazama Watakatifu kutoka sehemu hii akisema mfumo wao wa maisha ni mchango mkubwa katika kujifunza maisha yanayofaa kwa viongozi wa dini na furaha ya watawa wake kwa waume hasa katika Mwanga wa mwaka maisha yaliyowekwa wakfu, kuweza kuangazia zaidi uzuri na utakatifu wa kazi zao. Papa alieleza na kutaja baadhi ya Watakatifu akikumbuka Cyprian Mkuu, Mtakatifu Augustine, Mwenyeheri Charles de Foucauld, ambaye , mwaka 2016 itatimia mia ya kifo chake. Watumishi hao wa Mungu walitoa kila kitu chao kwa Mungu na kwa wengine sadaka ya maisha .








All the contents on this site are copyrighted ©.