2015-02-28 08:05:39

Padre Kyalembera ameuwawa!


Askofu Thèophile Kaboy Ruboneka wa Jimbo Katoliki la Goma, nchini DRC anasema kwamba, Padre Jean- Paul Kakule Kyalembera hivi karibuni aliuwawa kikatili Parokiani mwake, Mweso na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Marehemu Padre Kyalembera baada ya kuhitimisha shughuli na utume wake, jioni wakati wa kufunga mlango wa Kanisa, akagundua kwamba, kulikuwa na kundi la watu waliokuwa wamejificha Kanisa humo na walipomwona, wakafyatulia risasi na Padre Kyalembera kupoteza maisha yake Kanisa hapo! Tayari watu kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hili wamekwishatiwa mbaroni!

Askofu Ruboneka anasema, kwa muda mrefu eneo la Goma limekuwa ni uwanja wa fujo na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia kutokana na uwepo wa makundi ya kijambazi pamoja na kuzagaa kwa silaha: Mapadre na watawa wanaendelea kutishiwa maisha yao na wakati mwingine wanalazimishwa kutoa fedha, jambo ambalo ni hatari kwa maisha na usalama wa raia.







All the contents on this site are copyrighted ©.