Vita, fujo na ghasia vilipamba moto sana mwaka 2014
Mwaka 2014 unaweza kupewa sifa za kuwa mwaka wa ghasia za mapigano na fujo, zilizo
sababisha majanga kwa mamilioni ya watu walionaswa katikati ya ghasia hizo. Ripoti
ya mwaka ya Asasi ya Kujitegemea “ Amnesty International”, imeeleza baada ya kuchambua
hali ya utulivu na amani katika nchi 160 na kusema ni aibu utendaji wa kimataifa,
kushindwa kukabiliana na ghasia hizo na mauaji yanayo fanywa na makundi ya waasi.
Rais
wa Amnesty Italia, Antonio Marchesi , katika mahojiano na Francesca Sabatinelli, ameitaja
ripoti hiyo kuwa ni hali halisi, inayozungumzia ukweli wa moja kwa moja kwa maisha
ya mamilioni ya watu walio naswa katika migogoro yenye vurugu kuanzia Gaza, Nigeria,
Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Iraq, na mbele ya uso wa janga hili, jumuiya
ya kimataifa imebaki mbali. Mwaka huu umeongoza kwa dunai kushuhudia machafuko mengi
tokea miaka 70 iliyopita baada ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa. Dunia imeshuhudia
vurugu nyingi katika ngazi ya kimataifa zenye kusababisha wimbi kubwa na wakimbizi
na wahamiaji. Antonio Marchesim, ameeleza kwa kurejea taarifa mbalimbali za mwaka
2014, zinazoonyesha idadi kubwa sana ya mauaji yaliyofanywa na serikali na makundi
ya waasi, kwa njia vita, mfano mashariki mwa Ukraine, yaliyo rejesha Ulaya kuishi
katika mazingira ya Vita Baridi. Ongezeko la nguvu za makundi binafsi kama yale yanayodai
kupigania haki ya nchi kutawala kwa mtindo wa sheria za Kiislamu, kama vile Boko
Haram na Al Shabaab.
Rais wa Amnesty Italia anasema, “Jumuiya ya kimataifa
huwezi kujenga kuta, katika kulinda mipaka yake kwa mataifa kadhaa. Kuna dharura
ya kibinadamu na nchi tajiri zinao wajibu wa kuingilia kati mgogoro wa kiuchumi, na
nchi za kawaida na maskini pia lazima zifanye sehemu yake. Ameeleza kwa kutoa mfano
kwamba, watu wengi wamekimbia kutoka Syria na kuingia Lebanon, Jordan, Uturuki, katika
baadhi ya kesi nchini Iraq, si katika nchi za Ulaya. Wimbi hilo la wakimbizi haliwezi
kuitwa wimbi la uvamizi, maana watu hao wanakimbia madhulumu halisi dhidi ya maisha
yao.
Takwimu za mahusiano katika nchi 18 zimeonyesha kwamba, kumekuwa na
uhalifu wa kivita au ukiukwaji mwingine wa "sheria za vita". Na katika nchi 35 kumekuwa
na makundi ya waasi ya ukiukwaji wa haki na amani nakusababisha wakimbizi zaidi ya
3,400 na wahamiaji kufa maji katika bahari ya Mediterranean. Na wakimbizi 4 kutoka
Syria –asilimia 95% , wanaishi katika nchi jirani na katika nchi 119, kumekuwa na
vikwazo katika uhuru wa kujieleza. Amnesty International inataka si kupitisha mbinu
kibabe na kandamizi katika kukabiliana na unyanyasaji na madhulumu kwa sababu jibu
la nchi katika kukabiliana na vitisho hivyo , halipaswi kuhatarisha haki za msingi
za binadamu. Na kwa kuwa utumiaji wa mabavu hauwezi kuwa suluhu ya kudumu katika migogoro
mingi, anasema Marchesi.
Na hivyo, Amnesty International, imetoa wito kwa
Wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutoa mapema jibu
lao kwa ujumla, kupitia njia rasmi ya nguvu yao ya Veto, wakati wanapojadili hali
halisi za vurugu na mauaji ya kiholela au mauaji ya kimbari, ikiwemo adhabu zinazo
stahili kwa makosa hayo. Hatua nyingine ni kuridhiwa kwa mkataba wa biashara ya silaha,
ambayo imeridhiwa na nchi nyingi, lakini mataifa makubwa Marekani, Urusi, Canada,
Israel, hawajaridhia mkataba huo. Ni jambo muhimu kwa mataifa makubwa kuridhia mkataba
huu kama hatua muhimu katika kukomesha mzunguko wa silaha zenye kutumia kemikali za
hatari” arsenals”, ambazo huishia katika mikono ya watu na hivyo kuleta wasiwasi mkubwa,
wa kuangamiza maisha ya watu wengi wasiokuwa na hatia.