Tuzo ya Heshima ya Amani yamwangukia Esther Ibaga wa Nigeria
Tuzo ya Amani ya Heshima ya 32 ya Niwano, imemwangukia Esther Abimiku Ibanga, Mchungaji
na mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Nigeria, kwa kuchaguliwa kuwa mshindi
wa tuzo ya amani ya Niwano ya 32.
Jopo la uteuzi la kimataifa na Shirika
la Niwano Peace Foundation, limemteua Esther Ibanga , kwa kuridhika naye kwamba ,
si tu anatetea usalama wa maisha ya maelfu ya watu, lakini pia alianzisha shirika
lenye kugusa maelfu ya wengine." Esther Abimiku Ibanga, Machi ya 2010 alianzisha
Asasi inayo julikana kwa jina "Wanawake Bila Kuta" (Wowwi), kwa hamu ya kutaka kukomesha
vurugu na mauaji kwa wanawake na watoto, katika Jimbo la Nyanda za juu nchini Nigeria.
Asasi
hiyo ya kujitegemea, viongozi wake wametoka makundi yote ya kikabila Nigeria, na kama
ilivyo asili yake, limekuwa ni muungano wa nguvu wa vikundi vya wanawake , dhidi
ya mgawanyiko wa kikabila na kidini, muungano wa viongozi wanawake wakiwemo Wakristo
na Waislamu. Jukumu lake ni kuonyesha jinsi wanawake wanavyo paswa kuwajibika katika
kujenga amani.
Habari inafafanua kwamba, madhumuni ya juhudi hizi, ni kukuza
mbinu shirikishi na njia bunifu zinazoweza kuwaunganisha Wanigeria bila vurugu katika
kutatua migogoro ya kijamii na katika kufanikisha mageuzi Nigeria kupitia wanawake.
Na pia miongoni mwa mambo mengine, ni kuunda muungano wa nguvu wa vikundi vya wanawake
katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, dhidi ya aina yoyote ya mgawanyiko, pia kutoa
ufahamu juu ya umuhimu wa jukumu la wanawake katika kujenga amani. Juhudi hizi zimeutazama
ukweli kwamba, katika migogoro mingi ya Afrika, ikiwa ni pamoja na Nigeria, wanawake
na watoto huteseka kwa matokeo mabaya. Wakati huo huo, kama mama, wanawake ni waelimishaji
wa kwanza wa wanadamu. Katika hali hii, kazi ya Ibanga inalenga kukuza na kutumia
fursa za wanawake kama wapatanishi, na kutambua kwamba wanawake wanaweza kuwa na ushawishi
nguvu katika maisha ya watu (baba, ndugu, waume na wana).
Shirika hili la Ibanga
linakemea vikali utendaji wa kikundi cha Boko Haram. Na ili kuweka kufanikisha maono
na malengo yake katiak juhudi za Wanawake bila Kuta, chini ya uongozi wa Mchungaji
Ibanga, limechukua hatua za kuongeza nafasi za wanawake kwa njia upatikanaji wa ujuzi
na misaada midogomidogo ya fedha. Mara kwa mara limekuwa likiandaa maandamano na
bila kuchoka kutoa wito kwa viongozi wa serikali na wanasiasa, wajishughulishe zaidi
na suala la dhuluma na unyanyasaji kwa wanawake, likipaza zaidi sauti ya akina mama
na sauti chanya ya viongozi wa kidini dhidi ya wababe wa vita ambao wanatumia dini
kuhamasisha vijana kufanya vurugu ili kukidhi nia ya ubinafsi wao. Juhudi hizi
dhidi ya ugaidi na ujenzi wa amani, "Wanawake Bila Kuta” mara ya kwanza, huandaa mazungumzo
ya jamii na polisi, kwa nia ya kukuza uaminifu kati ya jamii na polisi katika jitihada
za kukabiliana na ugaidi. Pamoja na mashirika mengine pia kukuzwa amani na mshikamano
mashuleni, hasa katika mkoa wa Nyanda za Juu Nigeria, ambao umesongwa na madhulumu
ya Boko Haram. Asasi hiyo pia huwakilisha wanawake katika mikutano ya kimataifa na
vikao katika nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Rwanda, Afrika Kusini, Austria na
Marekani. mchungaji Ibanga pia alikuwa mmoja wa wawakilishi wa wanawake katika mikutano
ya Umoja wa Mataifa, uliozungumzia haja ya "kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji
na mauaji ya jinai dhidi ya makundi ya wachache".