2015-02-17 12:22:38

Askofu mkuu Adolfo Yllana ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Australia


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Adolfo Tito Yllana kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Adolfo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini DRC. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa kunako tarehe 6 Februari 1948 huko nchini Ufilippini.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 19 Machi 1972. Tarehe 13 Desemba 2001 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2002. Tangu wakati huo, ametoa huduma za kidiplomasia kwenye Visiwa vya Solomon, Pakistan na DRC.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.