Monsinyo Fernando Chica Arellano ateuliwa kuwa Mwakilishi wa Vatican: FAO, IFAD na
WFP.
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Fernando Chica Arellano kuwa Mwakilishi
wa kudumu wa Vatican kwenye: Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO,
Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo wa Umoja wa Mataifa, IFAD pamoja na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Mshauri
wa Ubalozi wa Vatican.
Monsinyo Fernando Chica Arellano, alizaliwa kunako tarehe
24 Juni 1963. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe
19 Aprili 1987. Baada ya kujiendeleza na kupata shahada uzamifu katika Mafundisho
tanzu ya Kanisa, alianza huduma ya kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe Mosi,
Julai 2002.
Tangu wakati huo ametekeleza utume wake kwenye Ubalozi wa Vatican
nchini Colombia, Ubalozi wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa na huduma kwenye Sekretarieti
ya Vatican kuhusiana na masuala ya jumla.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa
ya Kiswahili ya Radio Vatican.