Mameya kutoka Nchi Takatifu baada ya kuhudhuria Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko,
Jumatano tarehe 11 Februari 2015, wamekutana pia na kuzungumza na Kardinali Pietro
Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, wakionesha matumaini yao katika kukoleza mchakato
wa matumaini na amani katika Nchi Takatifu.
Viongozi hawa wamemshirikisha
Baba Mtakatifu: matatizo, changamoto na matumaini yao kwa Nchi Takatifu pamoja na
kulishukuru Kanisa kwa huduma ya upendo na mshikamano unaooneshwa kwa wananchi huko
Nchi Takatifu hasa katika sekta ya elimu, afya na huduma kwa jamii. Hospitali ya Watoto
iliyoko Bethlehemu inahudumiwa na Kanisa kwa njia ya fedha ya wafadhili kutoka sehemu
mbali mbali za dunia na kwamba, hii pia ni fursa ya ajira kwa wafanyakazi 238.
Hospitali
ya Watoto ya Caritas Bethlehemu, ina uwezo wa kulaza watoto 82 na kila mwaka watoto
wanaolaza Hospitalini hapo ni zaidi ya 4,000. Huu ndio utandawazi wa upendo, mshikamano
na udugu; utandawazi unaoguswa na mahangaiko ya jirani.
Na Padre Richard A.
Mjigwa, C.PP.S. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.