2015-02-10 15:13:43

Utafuteni uso wa Mungu!


Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican, Siku ya Jumanne, tarehe 10 Februari 2015, Kumbu kumbu ya Mtakatifu Scholastica, mtawa na Bikira, amewataka waamini kufanya hija ya maisha ya kiroho, ili kuutafuta uso wa Mungu, ili hatimaye, waweze kuwashirikisha wengine.

Wakristo wasiojishughulisha katika maisha yao, kamwe, hawataweza kuufahamu uso wa Mungu na hivyo kushindwa kumfahamu kwa ukamilifu zaidi. Hii ni hamu ambayo Mwenyezi Mungu amemwekea mwanadamu katika sakafu ya moyo wake, inayomchangamsha kumtafuta Mungu, ili aweze kuwashirikisha pia jirani zake. Utambulisho wa Mkristo unajionesha katika bidii ya kutafuta kutekeleza mapenzi ya Mungu kwa njia ya mapendo na utimilifu wa Amri zake.

Kamwe mapokeo ya watu kisiwe ni kikwazo cha kutekeleza mapenzi ya Mungu, kwani mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.