2015-02-09 09:12:42

Watawa shikamaneni!


Yafuatayo ni mahubiri yaliyotolewa na Padre Sostenes Luyembe, SJ, Mwakilishi wa Askofu kwa Mashirika ya Kitawa, Jimbo kuu la Dodoma kama sehemu ya ufunguzi rasmi wa Mwaka wa Watawa Duniani, ngazi ya Jimbo kuu la Dodoma.

Mwaka hadi mwaka , Kanisa hututangazia “miaka ya kikanisa”. Na kwa kurejea na kutafakari hati za mtaguso mkuu wa pili hususani hati ya mwanga wa mataifa na dikrii juu ya marekebisho ya maisha ya wakfu ambazo inaongelea maisha ya wakfu na kwa kuzingatia ushauri wa “Congregation for institute of conncecrated life and for society of apostolic life”, Papa Francisko ameutangaza mwaka huu wa Kikanisa kuwa mwaka wa maisha ya wakfu, vita consecrata!

Mwaka wa kikanisa kitaalimungu unatualika kujiuhisha na kujipyaisha kiroho, tutafakari kwa kina maisha ya Kristo mwokozi wetu, Kristo aliyeishi katika muda aliyetenda katika muda aliyefariki katika muda ili kumtoa mwanadamu kutoka kwenye muda na kumwingiza kwenye utukufu. Aidha kupitia ipindi maalum wakati wote Kristo anamwumba mpya mwanadamu katika uhalisia wake na mzunguko wake wa kimaisha na kumweka katika mipangilio ya kimungu . Kama wasemavyo : Kristo akiutakatifuza muda na kuufanya kuwa Sakramenti ya upyaisho wa kiroho na makuzi ya kiroho. Maudhui makubwa ya mwaka huu wa maisha ya wakfu ni upyaisho wa maisha yetu ya kiroho kama watawa wakati wote tukimrejerea Kristo – yeye ambaye ni jana , leo na daima.

Moja ya vyakula ambavyo watu wa nchi za Afrika Magharibi hukipenda sana kinaitwa “port pourri” – mchanganyiko maalum! Hist: Mchannganyiko wa maua yaliyokaushwa , na kuwekwa ndani ya combo ili kuleta harufu nzuri – ubora wake ni kwamba unapata kila kitu ndani yake – Ni mchanganyiko unaozaa kilicho bora. Nautafakari mkusanyiko wetu leo hii kama ”un portpourri” , mchanganyiko maalum ambao unaendelea kulilisha na kulistawisha Taifa la Mungu lililoko Dodoma. Ubora huu utazidi kuimarika, kutegemea na jinsi tunavyoendelea kuchangamana kwa pamoja , kila mmoja akileta haufu yake njema ndani ya jimbo .” Sense of communion – and close collaboration ! Tendency to work alone, and according to our spiritual heritage!”

Akautangaza mwaka huu kuwa Mwaka wa Watawa Duniani , Baba Mtakatifu Francisko anabainisha malengo makuu ya mwaka huu kuwa ni matatu kama ifuatavyo: kuyatafakari yaliyopita kwa moyo wa shukrani, kuyaishi ya sasa kwa moyo wa hamasa , na kukumbatia ya mbele kwa moyo wa matumaini Jana, leo na kesho: Jana: Katika kutafakari yaliyopita kwa moyo wa shukrani tunaaswa kurejea maisha wa waasisi wa mashirika yetu, karama, nia na malengo na majitoleo yao ili kujibu mahitaji ya kikanisa na kijamii kwa nyakati hizo.

Kama ilivyokuwa kichocheo kwao katika kuihubiri injili , karama za waanzilishi wetu zinapaswa kuwa kichocheo kwetu pia katika kipindi chetu. Aidha wote tunaelezwa na kuundwa na historia yetu inatupatia utambulisho, inaimarisha mwungano wetu au umoja wetu kama familia ya mungu, na pia utambuzi wetu wa uanashirika. Nialike tu kuwa macho na kile tunachokiita uukaji wa karama ndani ya karama – kuna “vikarama” vingi vinazaliwa na mara nyingine kutufanya tuvuke mipaka na kuwa nje ya karama mama za kishirika! Historia zetu wenyewe zizidi kuamsha ari za kupambana kwa ujasiri na mahitaji ya kiinjili ya nyakati zetu.

Leo: Kawaida tunapoyatafakari ya kale kwa umakini na unyofu wa moyo ndani yetu huamshwa ari mpya ya kuyaishi ya kale kwa nguvu mpya , kuendana na mazingira na mahitaji ya vipindi vyetu. Roho wa Bwana anaziongoza dhamiri zetu kujitafiti namna ya kuhuisha karama zetu na maisha yetu ya wakfu kwa kupambana na changamoto za kizazi chetu. Tunapewa changamoto ya kuutafakari uaminifu wetun katika kuioshi mashauri ya kiinjili na jinsi !. Mwaka huu utujaze maono mapya ya kuishiIinjili ya Kristo.

Kesho: Kama wasemavyo “there is always tomorrow! Kesho ipo wakati wote ! Kuitafakari jana na leo kunatuingiza katika kesho. Mwaliko ni kujaribu kutafakari changamoto na baadhi ya vitu vinavyotishia umbele wetu mito inazidi kupungua, mashirika mengi yamebaki na wazee, masuala magumu ya kiuchumi, utandawazi, mivutano na migogoro ya kidini, kebehi, tunazozipata kwa kuyachagua haya maisha.(Usiogope ningali pamoja nawe). Ni ujasiri upi tunaoupata tunapozitazama changamoto za huko mbele.Tunapaswa kujenga ujasiri wa kusonga mbele kupigana bila kushindwa , utangulizi sala ya Ekaristi.

“Quoing the Pope- who quotes Benedict XVI, I urge you not to join the ranks of the prophets of doom who proclaim the end or meaninglessness of the consecrated life in the church in our day:rather , clothe yourselves in jesus Christ and put on the armour of light – as Saint Paul urged(Cf. Rom 13:11- 14)” Tujichunge:Umbea, wivu, unafiki , maisha yasiyo na tija ndani ya jumuiya, (kuyaishi ili mradi). Like every one else, we have our troubles, our dark nights of the soul, our disappointiments and infirmities, our experience of slowing down as we grow older. But in all these things we should be able to discover perfect joy. For it is here that we learn to recognize the face of Christ , who became like us in all things, and rejoice in the knowledge that we are being conformed to him who, out of us did not refuse the sufferings of the cross.

Na Padre Sostenes Luyembe, SJ,
Vika wa Watawa Jimbo kuu la Dodoma, Tanzania.








All the contents on this site are copyrighted ©.