2015-02-07 15:12:15

Kanali Graf, mkuu mpya wa Vikosi vya Ulinzi mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Luteni Kanali Christopher Graf, kuwa mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama vya walinzi kutoka Uswiss, al maarufu kama Swissguars na kumpandisha hadhi ya kuwa Kanali. Taarifa zinaonesha kwamba, uteuzi huu unaanza rasmi tarehe 8 Februari 2015.

Kanali Graf, alianza huduma ya ulinzi na usalama mjini Vatican kunako mwaka 1987 na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Daniel Rudolf aliyeanza kufanya kazi mjini Vatican kunako mwaka 2008 na mkataba wake kumalizika rasmi tarehe 31 Januari 2015

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.