2015-02-05 15:42:25

Wokovu unaoletwa na Injili si tauhidi za mafanikio ya kidunia


Kanisa lazima kutangaza injili "katika umaskini," na kila anayetangaza Injili ni lazima awe na lengo pekee la kupunguza mateso ya maskini, na kamwe bila kusahau kwamba, huduma hii ni kazi ya Roho Mtakatifu na si ya nguvu za kibinadamu. Ni wazo msingi katika homilia ya Papa Francisko, aliyotoa wakati wa Ibada ya Misa Alhamisi hii, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta , ndani ya Vatican.

Mafundisho ya Papa yalilenga katika utendaji wa Yesu kwenye kuponya, kusamehe, ukombozi, na upungaji wa mapepo. Na kwamba ilikuwa ni utendaji wa kazi za kawaida kwa ajili ya Ufalme wa Mungu wakati akiwa hapa duniani, alipita sehemu mbalimbali, mijini na vijijini akitibu na kuwaponya wengi waliojeruhiwa kimwili na kiroho pia. Papa alieleza akilenga katika kifungu cha Injil, wakati Yesu anawatuma wanafunzi wake wawili wawili katika vijiji, kuhubiri, kuponya wagonjwa na kufukuza "roho chafu".

Papa aliendelea kutazama kwa kina, uponyaji wa majeraha ya moyo, ambamo Yesu aliwaamuru wanafunzi wake, wasichukue chochote pamoja nao, si chakula, wala mkoba, wala fedha katika mikanda yao. Papa amefafanua kwamba, hii ni kwa sababu, ni kuitangaza Injili kwa maskini, kwa sababu wokovu wa Injili si teolojia ya mafanikio". Si kitu kingine zaidi ya kuwa, ni habari njema ya ukombozi, kwa kila anayejisikia kudhulumiwa.

Na huo ndiyo utume wa Kanisa. Kanisa ni kwa ajili ya uponyaji na huduma, kama ambavyo yeye mara kwa mara hulifananisha Kanisa kama kituo cha zahanati, ambako wengi wanakwenda kupata huduma za kuponywa majeraha ya mwili. Papa alieleza na kuhoji ni watu wangapi waliojeruhiwa kiroho? Ni wengi. Kanisa lina uwezo wa kuponya majeruhi hao. Huo ndio utume wa Kanisa, kuponya majeraha ya moyo, kuifungua milango ya roho na kupata kuponywa bila kudaiwa malipo. Kwa hakika Mungu ni mwema, Mungu husamehe wote, Mungu ni Baba, Mungu ni saburi ya roho, na daima Mungu anasubiri kutoa huduma hii bure...Papa Francisko amesisitiza.










All the contents on this site are copyrighted ©.