2015-02-03 15:25:51

Usikivu na Utii ni msingi wa maisha ya kitawa -Papa


Jumatatu Majira ya Jioni Papa Francisko aliongoza Ibada ya Misa Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya Siku ya Siku Kuu ya Bwana kutolewa Hekaluni pia kwa ajili ya adhimisho la Siku ya Watawa Duniani, Ibada inayohudhuriwa na watu wasiopungua elfu saba.

Mahubiri ya Papa, yalilenga zaidi katika nguvu ya utii, kama jiwe kuu la msingi katika maisha ya kidini. Na kwamba , kudumu katika njia ya utii, huonyesha vyote viwili ukomavu wa hekima kwa mtu binafsi na maisha ya kijumuiya, na hivyo inawezekana kuziishi sheria na kanuni katika nyakati zote , kwa ajili ya uboreshaji zaidi ukweli, kama matokeo ya matunda ya hekima yanayotokana na usikivu na utii.

Homilia ya Papa iliendelea kuwataka wote walio tolea maisha yao sadaka katika kumtukia Kristo na kanisa lake, kufanya bidii zaidi ya kuwaleta watu wengine kwa Yesu, lakini kwanza kabisa maisha yao wenyewe yakiwa mfano mzuri wa furaha iliyomo katika kuishi na Yesu.

Papa alieleza kwa kurejesha tafakari zake kwa Mama Maria, wakati alipoingia hekalu akiwa amembeba mtoto wake tayari kumkabidhi wa Bwana , kama ilivyokuwa desturiyao. Papa alitoa ufafanuzi kwamba, hili linaonyesha jinsi Yesu alivyo thamaini kwa kwa unyenyekevu na utii, njia na kanuni za maisha ya kijamii ya watu wake. Na hivyo ndivyo inavyopaswa kwa wafuasi wake kuifuata njia yake kwa utii na unyenyekevu , kwa ajili ya kuingia katika umoja nae thabiti, njia mpya inayo ongoza katika maisha mapya yaliyo hai (tazama Ebr 10:20)l.

Papa amelitaja hilo kuwa utaratibu wao wote ambao wamechagua kuweka maisha yao wakfu. Ni kutembea katika njia hiyo ya maisha ya kila siku, kwa utambuzi kwamba ni njia isiyokuwa na mbadala mwingine zaidi ya kufuata kanuni na taratibu za mwanzilishi wa shirika au jumuiya , kutembea ndani yake kwa furaha na uvumilivu.

Papa aliendelea kuelekeza juu ya maisha yaliyowekwa wakfu akisema kuwa ni njia yenye kuwa na sura ya kukubali kuongozwa na hekima na karama za mwanzilishi, bila kusahau kuwa utawala huwajumuisha wote, kila mtu na daima katika misingi ya Injili. Na Roho Mtakatifu, katika ubunifu wake usio na mipaka, huwa na matokeo ya sheria tofauti za maisha wakfu, lakini bila kupoteza ukweli halisi kwamba wote ni wana wa Kristo, na hakuna kinachopaswa kupunguza moyo wa Upendo wa Injili katika kuhudumiana.

Kwa njia hii hiyo Papa alisema sheria ya maisha wakfu, huweza kufikia hekima yake na tabia yake ambayo si dhahania lakini ni kazi na zawadi ya Roho Mtakatifu. Na dalili ya wazi ya uwepo wa hekima ni furaha. Ndiyo, furaha ya kiinjili na kidini kama matokeo ya mchakato wa kukutana na Yesu ... Papa aliasa , iwapo walioweka maisha wakfu kwa Bwana wataonekana kuwa watu wa kuhuzunika kwa namna gani wataweza kuwa mashahidi wa kweli wa Injili ya furaha?.


Papa alieleza na kuomba kwa bwana zawadi ya hekima hasa kwa vijana ambao bado hawajapata uzoefu wa kutosha katika maisha wakfu ili waweze kuwa tayari kutembea katika njia ya utii na usikivu kwa Roho. Utii huu na usikivu, isiwe kinadharia, lakini chini ya mantiki ya Umwilisho wa Neno lililokuja kukaa kwetu : usikivu na utii kwa maono ya mwanzilishi, usikivu na utii kwa utawala halisi, usikivu na utii kwa Mkuu wa shirika, usikivu na utii kwa Kanisa. Ni usikivu na utii halisi, kwa watu wote.

Papa alieleza na kusisitiza "amana" ya karama za kila familia ya kidini kuwa ni agizo la pamoja, utii na hekima katika njia ya safari hii ya maisha ya kuwekwa wakfu. Kama ilivyokuwa kwa Maria na Simeoni , pia walioweka maisha yao sadaka ya kulitumikia kanisa pia wanatakiwa kumkumbatia Yesu Mkononi kwa ajili ya kukutana na watu na kujiweka katika fumbo lake Kristo, Papa Francisko alisisitiza. .








All the contents on this site are copyrighted ©.