2015-02-02 15:14:19

Papa ataja safari zake zilizo tayari bombani


Jumapili wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, akihutubia maelfu ya waamini waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, alitangaza safari yake ya kitume kutembelea Sarajevo Mji Mkuu wa Bosnia/Herzgovina, hapo Juni mwaka huu. Hii itakuwa ni safari nane ya kimataifa katika kipindi cha miaka yake miwili ya kuwa Papa.

Licha ya safari za kimataifa pia hivi karibuni anatarajia kutembelea mjini Naples Italia, tarehe 21 Machi, na Mwezi Juni atakwenda Turin, Kaskazini mwa Italia tarehe 21 Juni, kwa lengo la kushiriki Ibada ya onyesho la Sanda Takatifu. Aidha kwa mwaka huu Papa anatazamia kwenda Marekani Philadephia , kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Dunia wa Familia, uliopangwa kufanyika Septemba 22-27-2015. Mwanzoni mwa mwaka huu mwezi Januari alifanya ziara ya Kitume nchini Sri Lanka na Philippines.

Awali, Papa aliangalisha hotuba yake katika somo la Injili, ambamo alisisitiza mambo matatu makuu juu Neno la Mungu kwamba ni kusikiliza, kukubali na kutangaza. Alisema kwa kuyatazama maandishi ya Mwinjilisti Marko, yanayoeleza juu ya Yesu kurudi Kafarnaumu, uliokuwa mji mkubwa katika eneo la Galilaya, watu wa mji huo, bila kuchelewa wakusanyika mara moja katika sinagogi, kumsikiliza Yesu.

Yesu alianza kuhubiri Neno la Mungu bila kusita, wala kufikiria fikiria mbinu gani atumike au kama vifaa, au itakuwaje , lakini yeye alilitangaza Neno la Mungu kwa kuwa aliona ni hitaji muhimu kwa jamii ya mji huo. Na hivyo, aliliwasilisha Neno la Mungu, na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, watu walivutiwa kwa sababu Yesu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi.

Papa aliendelea kufafanua juu ya nini maana ya mamlaka akisema kwamba, kwa yesu alizungumza kwa lungha ya kawaida ya wakazi wa eneo hilo,na watu waliweza kusikia nguvu ya Neno la Mungu katika maneno yake, waliona uvuvio wa mamlaka ya Mungu mwenyewe katika Maandiko Mtakatifu. Yesu alitoa Neno la Mungu, lililo timilifu kwa kile alichokitaja, maana Neno la Mungu huenda sawia na mapenzi yake.

Lakini binadamu mara nyingi hutoa maneno matupu, mengi huwa ni porojo zisizo kuwa na uhusiano na ukweli. Lakini , Neno la Mungu huenda sambamba na ukweli, vyote viwili ni huwa ni kitu kimoja kwa mapenzi yake, kile kinachosemwa hutendeka pia kwa kadri ya mapenzi yake. anachosema na kutenda. Na hivyo ndivyo ilivyo Injili, ni Neno la Maisha.

Papa Francisko alieleza na kuasa kwamba, Neno la Mungu si uonevu wala kunyima raha watu, lakini ni kinyume chake, huwaweka watu huru wale, hawa wale ambao wamefungwa kama watumwa na roho mbaya nyingi za ulimwengu huu kama ubatili, uroho wa fedha, kiburi, ufisadi .... Injili huleta mabadiliko ya moyo, hubadilisha maisha, hubadilisha mwelekeo mbaya na kuwa nia njema. Injili ina uwezo wa kubadilisha watu, Papa Francisko alisisitiza, watu kusoma Injili kila siku, kwa kuwa ina nguvu ya kubadili maisha, huleta mabadiliko ya moyo.

Baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Papa pia aliikumbuka Siku ya Kitaifa ya Italia, kwa ajili ya Maisha, na kutoa shukurani zake kwa walioandaa tukio hili la kutetea maisha ya binadamu kwa watu wote, na hivyo kuzima nia zinazotafuta kukuza utamaduni wa kifo. Aidha Papa alipeleka salaam zake kwa Mkutano wa Dunia wa juu ya Elimu, unaofanyika hapa Vatican kwa Mada: “wajibu wa wote katika elimu kwa ajili ya utamaduni wa kukutana."








All the contents on this site are copyrighted ©.