2015-02-02 14:25:35

Askofu mkuu Thomas Luke Msusa ateuliwa kuwa Rais wa ECM


Taarifa kutoka katika mkutano wa Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi inasema kwamba, Maaskofu wamemchagua Askofu mkuu Thomas Luke Msusa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Msusa pia ni mwanachama wa Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM.

Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi, limewachagua pia Maaskofu watakaosimamia shughuli mbali mbali za maisha na utume wa Kanisa nchini Malawi, sanjari na kuwateuwa Maaskofu wawili watakaowakilisha Familia ya Mungu nchini Malawi katika maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya familia, yatakayofanyika mjini Vatican, Mwezi Oktoba, 2015.







All the contents on this site are copyrighted ©.