Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 31 Januari 2015 amemtumia salam za pongezi
Mheshimiwa Sergio Mattarella kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais Mpya wa Italia. Ni matumaini
ya Baba Mtakatifu kwamba, Rais Mattarella atatekeleza dhamana na utume wake kwa ajili
ya kujenga na kudumisha umoja wa kitaifa, amani na maridhiano nchini Italia.
Baba
Mtakatifu anamwombea Rais Mattarella neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ili
aweze kumwangazia katika kazi yake, kwa ajili ya mafao ya wengi kwa kuzingatia tunu
msingi za kiutu na maisha ya kiroho miongoni mwa wananchi wa Italia. Baba Mtakatifu
anapenda kumpatia baraka kwake binafsi na kwa taifa zima la Italia.
Na Padre
Richard A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.