2015-01-30 09:07:08

Mlipuko wa gari la mafuta wasababisha vifo vya watu 7


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, amewakumbuka na kuwaombea wale wote waliofikwa na ajali iliyotokea kwenye Hospitali ya Watoto mjini Mexico na hivyo kusababisha watu 7 kupoteza maisha yao, kati yao kuna watoto 3. Baba Mtakatifu anawaombea wote waliofikwa na msiba huu amani na nguvu ya kuweza kuhimili magumu wanayokabiliana nayo kwa sasa pasi na kukata tamaa.

Taarifa zinazonesha kwamba, watoto 3 waliofariki dunia ni kati ya watoto wachanga 22 waliojeruhiwa kutokana na mlipuko wa gari la gesi, uliotokea, Alhamisi, tarehe 29 Januari 2015. Gari lilikuwa limeegeshwa karibu na jiko, pembeni mwa Wodi ya wazazi, ambako kuna vitanda maalum kwa ajili ya kutunzia watoto wadogo. Taarifa zinaonesha kwamba, kuna mtoto mdogo mmoja ambaye ameokolewa kutoka kwenye kifusi cha majengo yaliyobomoka.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.