2015-01-26 08:24:25

Rais Lungu aapishwa nchini Zambia


Bwana Edgar Lungu aliyetengazwa kuibuka kidedea katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni nchini Zambia kufuatia kifo cha Rais Michael Sata, mwezi Oktoba 2014, ametangazwa na kusimikwa rasmi kuwa Rais wa Zambia, Jumapili tarehe 25 Januari 2015 mjini Lusaka baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Bwana Hakainde Hichilema wa Chama cha UPND.

Sherehe hizi zimehudhuriwa na Rais Robert Mgabe wa Zimbabwe, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi ya Nchi zilizoko Kusini mwa Afrika, ambaye amempongeza Rais Lungu kwa kupata ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Zambia. Rais Lungu kwa sasa anasema, ataelekeza nguvu zake kwa ajili ya utekelezaji wa nchakato wa Katiba Mpya, ili uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Zambia, hapo mwaka 2016, uweze kufanyika kwa kuongozwa na Katiba Mpya, ambayo imekuwa ni kilio cha wananchi wengi wa Zambia.

Rais Lungu anasema, ataendelea kukamilisha sera na mikakati ya maendeleo iliyoanzishwa na Marehemu Rais Michael Sata, ili kuwaokoa wananchi wengi wa Zambia ambao bado wanaogelea katika lindi la umaskini wa hali na kipato!







All the contents on this site are copyrighted ©.