I wapi haki, kunyamazisha sauti ya kidini katika huduma za afya ?
Bila sauti ya waamini kusikilizwa katika huduma za afya nani atatetea haki ya wanyonge?
Ni maoni ya Daktari Denis Hunnell, Mtalaam katika huduma za Afya, aliyoyaandika katika
makala yake ya tarehe 23 Januari na kunukuliwa ns shirika la habari za Zenit. Makala
yanaonya dhidi ya unyamazishaji wa sauti ya kidini katika huduma za afya , kwa maelezo
kwamba, bila imani kutumika katika uwanja wa huduma za afya, hapatakuwa na utetezi
wa huduma za Afya hasa kwa makundi ya watu wanyonge katikajamii, kama wachanga,
wazee na wagonjwa mahututi.
Dr Hunnel, amesisitiza kwamba, uhuru wa kidini,
hutoa fursa ya utendaji katika misingi ya imani ya mtu katika kila nyanja ya maisha.
Na kwamba Uhuru dhamiri zi zaidi ya muumini kuwa na uhuru wa kuhudhuria ibada, anayopenda.
Lakini huwa ni maisha ya kweli katika chaguzi za utendaji wa maisha, kwa mujbu wa
imani yake yenye kumuunganisha na maisha, familia, kitaaluma na kijamii, huku akishiriki
katika mazoea yake ya kiroho, akiongozwa na matakwa ya imani yake, na misingi ya
kuheshimu uhuru imani za wengine
Kwa bahati mbaya, ameonya daktari Hunell,
“ tamaduni na desturi hizi msingi, zinazidi kusongwa na tabia za kukosa uvumilivu
katika uhuru wa imani, kama ilivyo, kwa Wakristo wa Mashariki ya Kati na katika
sehemu nyingi za Afrika, waamini wanateswa na kuchinjwa na Waislamu wenye msimamo
mkali. Na katika ulimwengu wa Magharibi, tamaduni za kidunia, ingawa hakuna vurugu
na kuchinjwa hadharani, kuna shinikizo la kutaka kutokomeza haki za imani za kidini
katika maisha yote ya umma, kwa kuwa na sheria mbalimbali zinazogandamiza uhuru wa
dhamiri, kama ilivyo huko Uingereza mfanyakazi alifukuzwa kwa kukataa kukiuka maadili
yake ya kidini, kufungisha ndoa watu wenye jinsia moja.
Dr Hunell anaonya
kuwa karibu katika kila taaluma, kuna hatari nyingi za dhamiri i kugandamizwa au
kubaguliwa, na hasa katika taaluma ya utabibu. Wahudumu wa afya, wengi hulazimshwa
kushiriki katika utendaji ulio kinyume na maadili yao ya kidini, mfano hushurutishwa
kushiriki katika utendaji wa utamaduni wa kifo mfano utoaji wa mimba na eutanasia.
Wafanyakazi Katoliki, wanao wajibu wa kuzingatia Mafundisho Katoliki, yanayokiri
maisha yote ya binadamu, yana hadhi kubwa, tangu wakati mimba inapotungwa hadi wakati
wa w kifo cha kawaida na Wakatoliki waaminifu huilinda heshima hii katika kila nyanja
ya maisha yao, ikiwa ni pamoja na shughuli zao kitaalamu. Wafanyakazi Katoliki katika
huduma za afya, anaendelea kueleza, hutoa changamoto katika mifumo wa afya duniani
iliyo kinyume na utetezi wa maisha katika asilia yake , hasa katika kutetea makundi
ya wadhaifu , kama wale ambao bado kuzaliwa na wazee , kama imani yao inavyowataka.
Makala imeendelea kuangalisha katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisco,kwa
Siku ya Wagonjwa ya Duniani 2015, ambamo ameonye juu ya uongo unaofanyika kwa kutumia
mgongo wa ufanikisha huduma bora katika makundi ya kijamii lakini ukweli wake halisi
ni kuangamiza maisha ya watu dhaifu wasioweza kujitetea wenyewe kwa ushupavu, mfano
watoto wachanga wasiozaliwa bado, wagonjwa mahututi wasiojiweza wanao chaguliwa matibabu
ya eutanasia , au maisha ya wazee yanayokatishwa kwa kunyimwa huduma, kutokana na
uzee wao. Na pia hata wale wanaojaribu kutetea maisha ya watu hao, sauti yao hunyamazishwa
kwa vitisho vya kufutwa katika upeo wa huduma za afya za kijamii. Huku ni kunyamasisha
sauti ya imani katika huduma za afya .
Makala inaendelea kusema, bila imani
katika huduma za afya, nani ataweka breki kwa makampuni ya dawa yanayotafuta kutengeneza
dawa kwa manufaa yao binafsi? Wapo wengi wanaotaka kutengeneza dawa kwa lengo la
kuvuna utajiri bila kujali athari za maisha ya wengine.
Na Madaktari , Franklin
Miller na Robert Truog, wanasema, bila kuzingatia maadili ya kidini ni nani atakuwa
mtetezi wa maisha hadi kifo chake cha kawaida? Ni nani atakayekemea uvunaji wa viungo
muhimu kutoka kwa watu wengine na hasa walio wanyeonge katika jamii? Ni nani atakaye
simama dhidi ya mmomonyoko wa uhuru wa kidini katika huduma za afya na zaidi ya vishio
katika fani ya Maisha ya Katoliki katika huduma ya afya?. Hakuna isipokuwa ni misingi
ya maadili ya imani, kulindwa na kutambuliwa kama ni haki msingi katika nguvu ya kutetea
heshima na haki za watu binafsi dhidi ya urasimu tenge katika mizania ya heshima ya
maisha ya mtu.
Makala imehimiza walio katika uwanja huu wa huduma za afya na
hasa watalaam na wahudumu , kuuanza mwaka huu kwa kufanya kazi kwa bidii zaidi hasa
katika kupambana na wimbi la unyanyasaji wa imani ya kidini katika huduma ya afya.
Lazima dhamiri za kidini zilindwe na kutetewa na wataalam wote wa afya.