2015-01-26 08:52:53

Hatimaye, wameachiliwa huru!


Wamissionari wawili waliokuwa wametekwa nyara na watu wenye silaha huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, hivi karibuni, hatimaye, wameachiwa huru. Serikali ya Ufaransa imempongeza kwa namna ya pekee, Askofu mkuu Diedonnè Nzapailanga wa Jimbo kuu la Bangui, kwa jitihada zake ambazo zimewezesha wamissionari hao kutoka Ufaransa kuweza kuachiliwa huru.

Kwa sasa kuna juhudi zinazoendelea za kutaka kumwokoa Jenerali Andjilo aliyekuwa anaongoza kampeni dhidi ya Kikundi cha Balaka, aliyekamatwa tarehe 18 Januari 2015 na Vikosi vya Umoja wa Mataifa, vinavyofanya kazi huko Afrika ya Kati.









All the contents on this site are copyrighted ©.