2015-01-21 15:32:48

Papa aomba amani na mapatano Niger


Baba Mtakatifu Francisko, ameomba amani na mapatano kwa taifa la Niger, kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na kikundi cha Boko Haram. Papa ametoa wito huo, baada ya kukamilisha katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliokusanyika katika ukumbi wa Paulo VI wa hapa Vatican, mapema Jumatano hii.

Papa ameomba watu wote wenye mapenzi mema, kuombea mema taifa pendwa la Niger, na hasa kafara wa upinzani uliofanywa na kikundi cha Boko haram hivi karibuni nchini humo, madhulumu makubwa yaliyolegwa kwa Wakristo, watoto na makanisa. Na amemwomba Bwana, zawadi ya mapatano na amani ili kwamba dini kamwe isitumiwe kama chombo cha kuzua ghasia, maonevu na uharibifu. Na amekemea vikali kutumia jina la Mungu, kama sababu ya kuzua vita. Papa anatumaini amani na utulivu, vitarejea na kudumishwa Niger katika hali za kuheshimiana na kuishi pamoja kwa ajili ya manufaa ya wote. Na ametolea sala kwa Mama Bikira Maria, Malkia wa Amani kwa ajili ya watu wa Niger.

Wiki iliyopita, katika mji Mkuu wa Niamey, na mji wa Zinder , jumla ya watu 15 waliuawa na makanisa kadhaa kuchomwa moto na kuharibiwa katika ghasia zilizofanywa kikundi cha Kiislamu cha Boko Haramu, wakipinga picha za katuni zilicho chorwa na gazeti la Charlie la Ufaransa, zinazomwonyesha mtume Mohamed.Ghasia zilizodumu muda wa siku mbili.

Taasisi za usalama za Niger , zililazimika kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia ya watu waliojiunga katika uharifu huu ukiongozwa na kikundi cha Boko haramu.








All the contents on this site are copyrighted ©.