2015-01-21 15:46:54

Papa amshukuru Mungu kwa ziara yake ya kitume barani Asia


Jumatano hii , wakati akitoa Katekesi yake kwa mahujaji wa wageni katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican, Papa aliangalisha juu ya ziara yake ya kitume ya kimataifa ya saba, aliyoifanya huko Sri Lanka na Ufilipino wiki iliyopita. Ziara aliyoifanya baada ya kutembelea Korea miezi michache iliyopita, katika bara hili la Asia alilolitaja kuwa na utajiri mkubwa mila, utamaduni na kiroho pia .

Papa ameitaja ziara hii kwamba, imekuwa ni tukio lililomwezesha kukutana kwa furaha na jumuiya za kikanisa, katika nchi hizo, zinazoshumhudia Kristo, na ameweza kujionea mwenyewe imani na utume thabiti. Na kwamba, katika moyo wake daima atakumbuka jinsi watu wengi walivyofika kumlaki na kumsikiliza. Na kwamba katika kukutana na madhehebu ya dini nyingine , alihimiza zaidi mazungumzo ya amani, kama njia ya kuwaelekeza watu katika umoja na maendeleo ya jamii, hasa kwa familia na vijana.

Na pia ametaja jinsi ilivyokuwa furaha kwake , kukutana na jumuiya Katoliki , hasa kwa ajili ya tukio la kumtangaza kuwa Mtakatifu Mtumishi wa Mungu , Joseph Vaz huko Sri Lanka, aliyemtaja kuwa mfano wa utakatifu na upendo kwa jirani , anaye endelea kuhamasisha Kanisa Sri Lanka ,katika utume wake wa upendo na elimu, na katika mahusiano ya kuheshimiana na dini zingine. Mtakatifu Joseph Vaz, ni mfano hai wa kuigwa na Wakristo wote katika ukweli wa kuokoa wa Injili, na maisha ya uvumilivu na unyenyekevu. Papa anasema, Sri Lanka ni nchi ya kubwa yenye uzuri wa asilia, lakini bado inakabiliwa na mateso yanayotokana na vita ya miaka mingi. Hivyo katika mikutano na viongozi wa kidini aliwaomba kufanya kazi kwa kushirikiana , kwa ajili ya kufanikisha uponyaji wa majeraha ya nyuma , amani na maridhiano kwa manufaa ya wote.

Aidha Papa ameeleza kwa nini aliamua kwenda Ufilipino ,akisema ilikuwa kukidhi hamu yake ya kuwa karibu na kuonyesha mshikamano wake na wale walioathirika na Kimbunga cha Yolanda. Kwa ajili hiyo, aliongoza Ibada mjini Tacloban , kuomba huruma na faraja za Mungu kwa ajili ya wote walipondeka mioyo. Na akiwa Manila, alitoa wito wa familia kulindwa kama wajibu msingi katika maisha ya kijamii na ni mpango wa Mungu.. Na kwamba ilikuwa ni furaha kwake kukutana na vijana wa Ufilippino, kusikiliza matumaini yao na matatizo yao. Na alitoa mchango wake katika juhudi zao kwa kuwataka wachangie zaidi upya katika maisha ya kijamii na hasa kwa njia ya huduma kwa maskini na ulinzi wa mazingira ya asilia.
Amesema huduma kwa maskini ni nyenzo muhimu katika maisha ya Kikristo na shuhuda. Na kwamba katika ziara hii alirudia kukemea aina zote za rushwa, kwa sababu rushwa , hudhulumu maskini na utamaduni wa uaminifu. Papa aliwaomba watu wa Ufilipino kumwinamia msimamizi wa taifa lao ambaye ni Mtoto Yesu , akiwahimiza pia kutunza thamani ya ushuhuda wao kwa Injili katika bara hili kubwa la Asia.

Na alikamilisha kwa kumshukuru Bwana, kwa kuifanikisha ziara hii ya Kitume Sri Lanka na Philippines. Na ameyaombea mataifa haya wawili baraka za Bwana ili yadumu daima, katika kuthibitisha uaminifu wa Kristo na ujumbe wa injili ya kuokoa, maridhiano na ushirika na Kristo.








All the contents on this site are copyrighted ©.