2015-01-20 11:54:27

Matumaini katika mapambano dhidi ya Ebola!


Ugonjwa wa Ebola umewatikisa sana wananchi wa Sierra Leone, Liberia na Guinea, kiasi cha kuwaachia machungu ya watu kuondokewa na ndugu zao pamoja na kukwamisha mchakato wa ukuaji wa uchumi. Shirika la Afya Duniani, WHO linabainisha kwamba, kuna zaidi ya watu 21, 000 wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola na kwamba, zaidi ya watu 8, 400 wamefariki dunia.

Kwa sasa kuna habari njema kwamba, kwa takribani mwezi mzima, hakuna mgonjwa wa Ebola aliyejitokeza nchini Sierra Leone, habari ambazo zimepokelewa kwa matumaini katika mchakato wa kupambana na janga la Ebola huko Afrika Magharibi.

Hii ina maana kwamba, porotokali dhidi ya ugonjwa wa Ebola imeendelea kufanyiwa kazi na matokeo yake yanaanza kuonekana, ingawa waathirika wa ugonjwa wa Ebola wanapaswa kusaidia, ili kuanza tena hija ya maisha yao kwa matumaini zaidi baada ya kutembea gizani kwa miezi kadhaa tangu ugonjwa wa Ebola ulipozuka huko Afrika Magharibi.

Taarifa zinaonesha kwamba, ugonjwa wa Ebola umedhibitiwa pia nchini Mali na kwamba, hadi sasa hakuna tena mgonjwa wa virusi vya Ebola kutoka nchini humo. Mali ni kati ya nchi sita za Afrika Magharibi zilizokuwa zimetikiswa mno na virusi vya Ebola.







All the contents on this site are copyrighted ©.