2015-01-14 15:37:46

Sri Lanka yatoa msamaha kwa wafungwa 612!


Wakati wa hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Sri Lanka, serikali nchini humo, imetoa msamaha kwa wafungwa 612, kati yao kuna wanawake 37. Hayo yamebainishwa na msemaji mkuu wa Gereza kuu la Thushara Upuldeniya. Kundi la wafungwa lililofaidika na msamaha wa Rais wa Sri Lanka ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 75 pamoja na wafungwa ambao wamekuwa wakitumia adhabu yao kwa makosa madogo madogo.

Taarifa zinaonesha kwamba, tkuo hili limefanyika siku ya Jumatano, tarehe 14 Januari 2015 wakati Baba Mtakatifu anaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumtangaza Padre Joseph Vaz kuwa Mtakatifu, kiongozi aliyejipambanua kwa huduma ya upendo, msamaha, haki, amani na upatanisho kati ya watu.









All the contents on this site are copyrighted ©.