2015-01-14 15:28:49

Shukrani kwa Rais mstaafu Napolitano!


Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika hija yake ya kitume Barani Asia, amemtumia salam za matashi mema, Bwana Giorgio Napilitano aliyekuwa Rais wa Italia baada ya kung'atuka kutoka madarakani siku ya Jumatano tarehe 14 Januari 2015. Baba Mtakatifu anampongeza Rais mstaafu Napolitano kwa huduma makini aliyoitoa kwa wananchi wa Italia bila ya kujibakiza kwa kuonesha uaminifu na uadilifu, kwa ajili ya mafao ya wengi.

Baba Mtakatifu anampongeza Rais mstaafu Napolitano kwa hekima na busara katika kukuza na kudumisha mshikamano, umoja wa kitaifa, amani na utulivu mintarafu Umoja wa Ulaya, hata kama Italia imeguswa kwa namna ya pekee na matatizo pamoja na changamoto nyingi. Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha ujumbe wake kwa kumwahidia Rais mstaafu Napolitano neema na baraka na kwamba, ataendelea kumkumbuka katika sala zake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.