2015-01-14 12:29:25

Rais Napolitano wa Italia ang'atuka kutoka madarakani!


Bwana Giorgio Napolitano mwenye umri wa miaka 89 baada ya kuiongoza Italia kwa kipindi cha miaka tisa, Jumatano tarehe 14 Januari 2015 amewasilisha Bungeni barua yake ya kung'atuka kutoka madarakani na hivyo kuacha nafasi kwa Waziri mkuu wa Italia Bwana Matteo Renzi kuanzisha mchakato wa kumpata Rais mpya wa Italia. Wananchi wengi wa Italia wanaoishi mjini Roma walimiminika kwenye Ikulu ya Italia, kumwaga Rais Napolitano ambaye wengi wanamsifia kwamba, amejitahidi kuiongoza nchi kwa moyo wa uzalendo na uadilifu mkubwa!

Tangu leo, Bwana Napolitano si kiongozi tena wa Italia na amehamia kwenye makazi yake binafsi. Anakumbukwa sana na wananchi wa Italia kwa kipaji cha akili, uaminifu na kwamba, alikuwa ni mtu huru aliyekubalika na wengi katika shida na magumu ambayo Italia imepitia katika historia na maisha yake.

Bwana Napolitano alikuwa ni mkweli na mtu wazi kwa maneno na matendo yake kamwe hakupenda "longolongo za kisiasa".







All the contents on this site are copyrighted ©.