Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vatican
Mheshimiwa Philip S. Marmo, Balozi wa Tanzania mjini Vatican katika mahojiano maalum
na Radio Vatican anapembua kwa kina na mapana mafanikio yaliyokwisja patikana nchini
Tanzania katika medani mbali mbali za maisha. Anazungumzia pia mgogoro ulioibuliwa
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kutaka kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislam,
OCIC na mchakato wa Muswada wa Katiba inayopendekezwa, ili kupata ufumbuzi wa masuala
kadhaa kwa Zanzibar.
Kwa namna
ya pekee kabisa, Balozi Marmo anajadili umuhimu wa Tanzania kuwa na mahusiano ya Kidiplomasia
na Vatican, au kwa kitaalam "Holy See" ambayo kwa sasa iko chini ya uongozi wa Baba
Mtakatifu Francisko, kwa kutambua kwamba, hii ni Jumuiya kubwa ya waamini ambayo ina
mchango mkubwa katika sera na mikakati ya kimataifa na kwamba, mchango wake unathaminiwa
sana na Jumuiya ya Kimataifa kama iliuvyojitokeza hivi karibuni kwa suluhisha mgogoro
wa kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa
ya Kiswahili ya Radio Vatican.