2015-01-11 13:35:04

Papa- Naomba mnisindikize kwa sala wakati wa ziara yangu Sri Lanka na Ufilipino,



Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili wakati wa adhuhuri, baada ya kutoa hotuba na sala ya Malaika wa Bwana, ameomba waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wamsindikize kwa sala na maombi, wakati wa safari yake ya kitume , anayoianza Jumatatu Jioni kwa nia ya kutembelea mataifa mawili, Sri Lanka na Ufilipino. Ziara itakayomchukua muda wa wiki nzima, Jumatatu 12-19 Januari 2015.
Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa alitoa maelezo juu ya Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana, ambayo imehitimisha kipindi cha Krismasi. Amesema, ubatizo wa Yesu si tu mpasuko wa kufungua milango ya mbinguni, lakini Mungu anarudia kutaja upya kwa sauti yake: "Wewe ni Mwanangu, mpendwa, na nimependezwa nawe" (Marko 1:11). Papa alifafanua ni Sauti ya Baba inayotangaza siri ya mtu anayebatizwa na Yohana Mbatizaji. Yesu, Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili, pia Neno la mwisho kutoka kwa Baba alilotaka kuielezea dunia. Hivyo ni tu kwa kusikiliza, kufuatia na kushuhudia Neno hili, inawezekana kikamilifu kutoa matunda ya uzoefu wa imani, ambamo mbegu iliyowekwa ndani ya mioyo yetu wakati wa ubatizo wetu huweza kuchipua.

Papa aliendelea kutoa tafakari juu ya kushuka kwa Roho Mtakatifu, kwa umbo la njiwa, akisema, inamshuhudia Kristo, kuwa mtiwa mafuta wa Bwana. Ni tukio linalo zindua kazi ya kutangaza ujumbe wake wa kuokoa kwa ajili yetu sote.Papa amemtaja Roho Mtakatifu kwamba ni Mhamasishaji wa maisha na huduma ya Yesu.

Ni Roho huyo anayeongoza maisha ya Kikristo. Papa ametoa wito kwa waamini wote, kuweka kila utendaji chini ya Roho Mtakatifu katika maisha yao kama Wakristo na wajumbe wa Neno la Mungu, ili kama walivyo mpokea katika Ubatizo, waendelee kupata ujasiri wa kitume, hasa katika kuyashinda kirahisi majaribu ya kidunia. Amesema, Mkristo na jumuiya isiyo sikia sauti ya Roho Mtakatifu, isiyokuwa na msukumo wa kupeka Neno la Injili hadi miisho ya dunia, huwa ni Mkristo na jamii "bubu" isiyozungumza wala kuinjilisha. .

Papa alieleza na kutoa maombi kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na wa Kanisa, kuongozana wabatizwa wote katika hija ya maisha, awasaidie waamini wa mwanae kukua katika upendo wa Mungu na katika furaha ya kuwa wahudumu wa Injili, na hivyo kuiona maana kamili ya maisha duniani.








All the contents on this site are copyrighted ©.