Wafukuzwa kwa kukataa kukana Ukristo - Mosul Iraki
Wazee kumi Wakaldayo Wakristo Wakatoliki wa Syria , wamefukuzwa kutoka eneo lao na
Wanamgambo wa kujitegemea wanajihadi wa Kiislam, waliozingira vijiji katika uwanda
wa Ninawi Iraki. Katika eneo hilo, kuna makazi ya pili kwa ukubwa la watu wanaokimbia
ghasia na mauaji yanayofanywa na wanajihadi hao.Wazee hao walipewa amri ya kuondoka
mara moja, baada ya kukataa kuikana imani yao ya Kristo, wakitakiwa kuongokea Uislamu.
Wazee
hao walikumbwa na mkasa huo wa kufukuzwa siku ya Jumatano,licha ya baadhi yao kuwa
katika hali mbaya za afya. Wazee hao wamepokelewa katika kambi ya Kirkut, baada ya
mwendo wa siku mbili katika hali ya baridi na bila kukutana na mtu yeyote na hawakuwa
wamechukua kitu chochote cha kuwafadhili kwa kuwa hawakuruhusiwa kufanya hivyo na
askari hao wanajihadi, waliojitangazia himaya yao ya kiislamu katika eneo walilolitwaa
la Ukrudi ya Peshmerga.
Mmoja wa wazee hao ameshuhudia kwamba , baada ya
mwendo mrefu na uchomvu mwingi, hatimae walipata msaada wa kutoka familia ya kiislamu
iliyowafadhili kwa chakula na mahitaji mengine muhimu. Wazee hao wametoa shukurani
zao kwa Patriaki Raphael Louis Sako, kwa kuiomba serikali ya kiraia, iondoe vipingamizi
kwa wazee, wanaopenda kuingia Kirkut kwa sababu za kiusalama . Pamoja na wazee 10
, pia ilikuweko familia moja ya Kiislam.