2015-01-10 14:52:37

Utume wa kwanza wa Kanisa ni kumsaidia binadamu kikamilifu –Papa


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi hii 10 Januari 2015, amekutana na wajumbe wa mkutano ulioitishwa kwa lengo la kutathimini hali ya waliopatwa na maafa ya tetemeko la aridhi, katika kisiwa cha Haiti miaka mitano iliyopita. Mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Pius X wa mjini Vatican, chini ya jina: Mshikamano wa Kanisa na matumaini kwa Haiti, Miaka mitano baada ya tetemeko la ardhi.

Mkutano uliandaliwa na Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki "Cor Unum" na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini, kwa kushirikiana na Maaskofu wa Haiti, kama yalivyokuwa mapenzi ya Baba Mtakatifu kuonyesha ukaribu wake kwa wahanga wa tetemeko hilo. Mkutano umeangalia matokeo ya utekelezaji wa miradi tangu mwaka 2010 hadi leo.

Wajumbe katika mkutano huu ni wajumbe wawakilishi kutoka Kiti Kitakatifu, Kanisa la Haiti, Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Oceania, wasimamizi wa mashirika ya Katoliki ya hisani, mashirika ya kidini, na wawakilishi mbalimbali wa kidiplomasia kwa Jimbo Takatifu. Mwenyeji wa Mkutano akiwa Kardinali Marc Ouellet, Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini, na Kardinali wa kadi. Robert Sarah, Mons. Giampietro Dal Toso, katibu wa Halmashauri ya Kipapa "Kor Unum". Na majira ya jioni, katika Kanisa la Mtakatifu Maria la Traspontina ,Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, itaongoza Ibada ya Misa, kwa ajili ya kuhitimisha, mkutano huo.

Hotuba ya Papa Francisco kwa mkutano huu, imesisitiza juu ya utume wa Kanisa kwamba ni kumsaidia binadamu kikamilifu. Papa alieleza kwa kuanisha na sherehe za Krismasi, akisema Umwilisho wa Mwana wa Mungu kuzaliwa katika hali ya kibinadamu , unatueleza umuhimu wa mahusiano ya mwanadamu na Mungu, aliye chukua asili ya mwanadamu. Hivyo utendaji wa kwanza wa Kanisa inakuwa lazima kumsaidia kila mtu, kuishi kikamilifu kama mtu.

Hakuna ujenzi halisi wa nchi bila ya ujenzi wa mtu katika ukamilifu wake. Ukweli huu pia ni kwa kisiwa cha Haiti, kwamba juhudi zote za maendeleo ni lazima manufaa ya wote kuwa kiini cha majadiliano. hii inasaidia kuhakikisha kwamba, kila mtu nchini Haiti ana umuhimu katika kusikilizwa maoni yake, anayoweza kuyatoa kwa uhuru kamili hasa kwa ajili ya ufanikishaji majukumu yao na maisha yao ya kiroho na kijamii.

Papa aliendelea kusema, binadamu ana upeo wa macho ya mbali, na ni haki yake , na Kanisa linapaswa kumsaidia mtu kuuona upeo huu, unaolenga kukutana na Mungu. Kwa hiyo, hata katika hatua hii ya ujenzi, kazi za kibinadamu na Kichungaji inakuwa si ushindani, lakini ni nyongeza, katika kukidhi mahitaji ya kila mmoja: kuchangia pamoja na kuunda raia wa Haiti waliokomaa, na Wakristo walio tayari kuhudumu kwa manufaa ya ndugu zao. Kwamba kila aina ya misaada inayotolewa na Kanisa na serikali , iweze kuunganishwa kwa ajili ya manufaa ya kumshirikisha kila mtu.
Papa aliendelea na kutaja kipengere kingine muhimu cha pili kwamba ni ushirikiano ndani ya kanisa. Na alionyesha kufurahi kwamba, kisiwani Haiti, kuna ushirikiano mzuri wa Kanisa kupitia ofisi zake tangu kijimbo, taasisi za kidini, mashirika ya hisani –na pia waamini wengi binafsi. Kila mmoja amejitokeza kwa sura ya kipekee, yenye kutoa umuhimu kipekee katika kazi ya kutoa misaada. Papa ametaja hii ni ishara ya uhai wa Kanisa na ukarimu wa watu wengi.

Papa alimemshukuru Mungu, ambaye amesimika katika wengi, hamu ya kuhudumia wengine kwa ukaribu zaidi, wakifuata sheria ya upendo ambayo ni moyo wa Injili. Na hata hivyo akaongeza, ushirikiano wenye upendo wa kweli si tu kusaidia wengine, lakini huwa na mwelekeo wa kujipenyeza katika hali zote za maisha, ukivivunja vikwazo na vizingiti vyote vyenye kutaka kuzuia moyo wa kukutana na wengine.

"Fadhila ni maisha halisi kwa Kanisa na ni wazi katika ushirika wa kanisa. Ushirikiano kati ya Maaskofu kwa Maaskofu, ni wajibu msingi kwa ajili ya huduma ya upendo, kama ilivyo ushirikiano kati ya Karama na karama na taasisi za upendo mbalimbali, ili kwamba kusiwe na mmoja anayefanya kazi kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe, lakini kwa jina la Kristo, ambaye mwenyewe alionyesha njia ya huduma. Papa alieleza na kuonya kwamba ni vigumu kuuishi upendo kwa kutengwa! Na hivyo alitoa wito kwa wote kuimarisha mbinu , na moyo wa e kufanya kazi kwa pamoja.

Papa alihitimisha hotuba yake akisisitiza umuhimu wa kanisa mahalia, lenyewe kuwa na utambuzi dhahiri, nini maana ya maisha ya Kikristo. Ni muhimu kwamba, Kanisa kisiwani Haiti litaweza kupata zaidi na zaidi matunda hai, kupitia ushuhuda wake kwa Kristo na kupitia mchango wake katika maendeleo ya nchi ya Haiti. Na hivyo Papa amehimiza Maaskofu wa Haiti, Mapadre na wafanyakazi katika huduma za Kichungaji , ushirikiano na bidii zao ziweze kuamsha ari ya mpya katika malezi ya Kikristo na Uinjilishaji. Alibaini, ushuhuda wa upendo wa Kiinjili, hupata kuwa fanisi pale unapodumisha mahusiano ya mtu na Kristo, kwa njia ya maombi, kusikiliza Neno la Mungu na katika njia ya sakramenti. Hapo kuna nguvu ya Kanisa mahalia.

Papa alirudia kutoa shukurani kwa kila mmoja wao , akiwasihi waendelee kutembea katika njia nzuri walioianza, na aliwahakikishia ya maombi yake ya mara kwa mara na baraka zake za kitume. Na Mama Yetu Bikira Maria , awaongoza na kuwalinda daima. Papa pia alisema anahitaji maombezi yao.








All the contents on this site are copyrighted ©.