2015-01-10 15:05:18

Askofu mkuu Eugene Martin Nugent, ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Haiti!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Eugene Martin Nugent, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Haiti. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Nugent alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Madagascar, Mauritius, Seychelles na Visiwa vya Comoro. Askofu mkuu Nugent alikuwa pia ni mwakilishi wa kitume wa Visiwa vya Riunione.

Uteuzi huu umefanywa na Baba Mtakatifu Francisko wakati Kanisa la kiulimwengu linafanya tathmini ya kina kuhusiana mchakato wa ujenzi wa Haiti mpya baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi yapata miaka mitano iliyopita. Wakati wote Kanisa limeonesha upendo na mshikamano kwa wananchi wa Haiti kwa njia ya misaada ya hali na mali iliyokuwa inasimamiwa na Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki, Cor Unum.







All the contents on this site are copyrighted ©.