Ziara ya Kitume ya Papa Francisco Sri Lanka na Ufilipino
Baba Mtakatifu Francisco, wiki ijayo, atakuwa na ziara ya kitume kwa muda wa wiki
moja, kutembelea mataifa mawili, Sri Lanka na Ufilipini, tangu Jumatatu hadi Jumapili,
12-19 Januari 2015. Kwa mujibu wa ratiba Papa ataianza safari Jumatatu tokea uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Fiumicino Roma hadi Colombo, Mji Mkuu wa Sri Lanka , mwendo
wa saa 9 na dakika 40 hewani, akipita katika anga za Italia, Albania, Ugriki Uturuki,
Irani, Shirikisho la nchi za Kiarabu, Oman, India na hatimaye Sri Lanka. Kutokana
na tofauti za saa, ndege ya Papa itatua katika uwanja wa ndege wa Colombo Siku ya
Jumanne. Katibu wa Vatican , Kardinali Parolin, katika mahojiano na vyombo vya
habari juu ya ziara hii ya Papa , amesema kuwa Papa aìinalenga katika mambo mawili
muhimu kwa ajili ya utume wa Kanisa barani Asia, kwanza ni kuhimiza matendo ya hisani
katika uwanja wa afya na elimu na pili, ni umuhimu wa kukazia mazungumzo kati ya
dini kama chombo muhimu kwa ajili ya amani katika dunia ya leo na hivyo unakuwa ni
wajibu kwa dini zote.
Kardinali Parolin, alieleza hilo hasa akilenga kujibu
swali lililoulizwa, iwapo Papa Francisko anarudi Asia na ujumbe mpya, katika mtazamo
kwamba, imepita muda wa miezi mitano tu tangu alipofanya ziara Korea, ambako katika
mazungumzo yake alikazia Kanisa kujikita katika majadiliano kati ya dini.
Kardinali
aliendelea kufafanua kwamba, utume wa Kanisa, iwe ufilipino , au Sri Lanka na duniani
kote: ni kutangaza Injili, kutangaza habari njema ya Yesu ambaye ni chanzo cha maisha
na matumaini ya watu wote. Utume unaofanywa na Kanisa kwa kuzingatia bila shaka,
mazingira linamoishi na kufanya kazi. Ni mazingira tofauti tofauti kutokana na
kwamba kanisa huundwa jamii mahalia bila kujali mchanganyiko wa jamii kikabila,
kitamaduni na dini. Na bara la Asia ni mbeleko ya dini kuu za ulimwengu. Na kwa kuzingatia
ukweli kwamba kanisa lina wafuasi wachache, ni kundi dogo, lakini katikati ya ukweli
wake ni kundi kubwa katiak maana ya utendaji wake. Na hivyo, bila shaka Papa atatoa
ujumbe wake, kulingana na sifa hizo.
Kardinali anasema Papa anaifanya ziara
hii, kama hatua ya kuwatia shime Wakristo wa Asia pamoja na uchache wao, kuona wana
umuhimu mkubwa katika ufanikishaji wa nyanja mbalimbali za maendeleo ya binadamu,
katika vyote kihali na kiroho pia hasa kupitia misaada katika uwanja wa afya na elimu,
ambavyo, tayari vinafurahiwa na kupokelewa kwa shukrani kubwa na watu wote na serikali
za nchi mbalimbali.
Kwa upande mwingine , Papa analenga kuhimiza zaidi mazungumzo
kati ya dini , kwa ajili ya kukuza na kuimarisha zaidi na zaidi, watu kukutana kwa
heshima, kukubalika na kuheshimiana, kama alivyoeleza katika waraka wake wa kitume
wa Injili ya Furaha, kwamba, mazungumzo kati ya dini, ni muhimu kwa ajili ya amani,
katika dunia ya leo na hivyo, unakuwa ni wajibu wa dini zote. Hoja hizi zitakuwa kitovu,
cha hotuba za Papa , katika ziara hii.
Kati ya matukio muhimu yatakayofanywa
na Papa Francisko katika ziara hii, ni Siku ya Jumanne , atakutana na kuzungumza na
wawakilishi wa dini mbalimbali katika kituo cha Congress cha mjini Colombo. Jumatano
ataongoza Ibada ya Misa kwa nia ya kumtaja Mtakatifu, Padre mahalia , Ibada itakayo
fanyika katika uwanja wa Gale Face Green mjini Colombo. Na jioni ataongoza Ibada
ya Rosari katika Madhabahu ya Madhu.
Alhamisi, Papa atasafiri hadi Manila
Ufilipino, ambako Siku ya Ijumaa , ataongoza Ibada ya Misa katika Kanisa Kuu la Mjini
Manila,Ibada itakayohudhuiwa na Mapadre na Watawa, na baada ye jioni kukutana na familia
katika ukumbi mkuwa wa Manila. Jumamosi Papa ataongoza Ibada ya Misa katika uwanja
wa ndege wa Tacloban , na baadaye jioni kukutana na Mapadre, Watawa, Wasemnaristi
na familia za kafara wa kibunga kaiak Kanisa Kuu la Palo. Jumapili ikiwa ni siku
ya mwisho ya ziara , asubuhi atakuwana na vijana na jioni ataongoza Ibada ya misa
katika uwanja wa Rizal wa mjini Manila.
Askofu Joseph Ponniah wa Jimbo la
Batticaloa, Mashariki mwa Sri Lanka, naye katika mahojiano anasema, Waamini Wakatoliki,
wamejawa na furaha isiyo kifani , kwa kuwa na Papa kwa muda wa siku tatu kisiwani
humu kutoka Januari 13-15. Na wengi wana hamu kubwa ya kusikia ujumbe wa matumaini
na maridhiano kutoka kwa Papa, kwa sababu wengi wana majeraha ya siku muda mrefu,
kutoka mbio za vita vya wenyewe kwa wenyewe, taifa bado kuponywa hasa na majeraha
yaliyoachwa na wanamgambo wa Tamil. Askofu ametajakti ya tukio la kuwasisimua
kiroho , ni ibada itakayoongozwa na Papa kwa ajiliya mkutaja kuwa mwenye Heri, Joseph
Vaz, aliyeishi karne ya 17, Padre kutoka India ambaye alifanya kazi kubwa, katika
kuijenga jamii Katoliki Sri Laka baada ya miaka mingi ya madhulumu na mateso. Askofu
Ponniah alionyesha furaha kubwa kwa mmoja wao kutajwa katika daraja hili la utakatifu
, akismea Wasyri Lanka wanamatumaini ya kusikia kutoka kwa Papa ujumbe wa amani na
maridhiano, neno wanalotamani kwa muda mrefu kulisikia baada ya miongo mingi ya vita
vya kiraia na mateso mengi yaliyo fanywa na vita hiyo. Pamoja na matumaini hayo,
Askofu Ponniah pia alionyesha kuwa na wasiwasi wa hali itakavyokuwa , baada ya matokeo
ya uchaguzi wa rais, kutangazwa katika uchaguzi unaofanyika siku chache kabla ya Papa
kutembelea taifa hilo. Baadhi wanahofu matokeo yanaweza kuleta mtafaruku , lakini
wengi wanaimani kwamba, kwa vyovyote itakavyokuwa katika matokeo ya uchaguzi huo,
amani na utulivu vitaendelea kutawala.