2015-01-05 10:58:35

Umeiona nyota angavu?


Epifania ni sikukuu ya mwanga na mwanga huo ni Yesu Kristu, mwanga unaoangaza. Mwangaza huo umewaangaza watu wote na unaendelea kuangaza. Ni sikuu ya mafumbo ya utoto wa Yesu (Rej. KKK 528. Mamajusi ni watu wenye busara wa mashariki ambapo baada ya kuiona nyota na kwamba bwana amezaliwa, walienda Yerusalemu kumwabudu. Zawadi walizochukua zilipatikana huko kwao – Yer 6,20. mababa wa kanisa waliona kuwa dhahabu ni mfano wa ufalme wa kristo, uvumba ulionya umungu wake na manemane ikionya mateso yake. Mamajusi walimsujudia kristo na ndivyo walivyotumia maneno ya Mungu juu ya Masiya kwamba mataifa watamwabudu Mungu wa Israeli Hes 24,17.

Ni mwanga kwa watu wote wanaomwendea Mungu wakiongozwa na imani ya huyo Mungu mwenyewe. Katika Isaya 60:1-6 tunapata habari juu ya utukufu wa Bwana unaong’aa Yerusalemu (ambao neno wa Mungu utatokea) mahali ambapo patakuwa ni makutano ya watu wote ili kumtukuza Mungu na kumtolea ubani na manemane. Katika barua kwa Waefeso 3,2-3,5-6 tunaona kuwa kwa Waebrania walioteuliwa kwanza na kwa wapagani waliokuja baadaye wote wameitwa katika imani moja kumfuata kristo na kugawana urithi wa milele pamoja naye. Wokovu wa Mungu ni kwa ajili ya ulimwengu mzima.

Katika Injili Mt 2,1-12 kutokujali na ujinga wa walimu na wakuu wa sheria, hofu na wasiwasi wa Herode imekuwa maangamizi kwao. Jibu sahihi la mamajusi tumeona nyota yake mashariki na tumekuja kumwabudi limekuwa wokovu wao. Wanatoka mbali na wanapata wokovu ila walio karibu hawatambui kuwa mwokozi amezaliwa.

Maana nyingine ya Epifania ni kujionyesha au kujifunua. Kwa maana hiyo ya kigiriki katika dini yao ilikuwa ni desturi kwa mmoja wa miungu kumtokea mmoja wao. Katika maandiko matakatifu neno hilo halipo bila shaka ni kuepa kuoanishwa na neno hili la kipagani. Tukisoma tu 1 Mak 1,10 tunaona helenistick king antioochus Epiphanes anayejifananisha na Mungu anayejionyesha.

Kiyunani Epifania twaona kuwa maneno hayo yaelekezwa kwa Yesu na kazi yake ya wokovu mpaka siku mwisho. 2 Tim 1:10- na sasa inadhihirishwa yaani neema ya Mungu kwa kufunuliwa kwake mwokozi wetu yesu kristo Yesu aliyebatili mauti na kuufunua uzima wa kutoharibika, kwa ile injili. Tito 2,11 maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunguliwa Tito 3,4 lakini wema wake mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa alituokoa.

Katika Kanisa jina hili Epifania limeonekana karne ya tatu likitumiwa kwa Yesu hivyo hatari ya kuhusishwa na upagani ikaisha kwa kweli Yesu ndiyo ufunuao wa Mungu. Kanisa la Mashariki likawa la kwanza kusherehekea sikuku ya tokeo la Bwana likiunganisha na ubatizo wa Yesu pale Mto Yordani. Itakumbukwa kuwa katika tukio hilo sauti toka mbinguni ilisikika ikasema huyu ndiye Mwanangu mpendwa wangu niliyependezwa naye msikilizeni yeye Mk 1:11 Mungu kwa mara ya kwanza anajifunua kuwa yeye ni nani kwa njia ya Yesu Kristo mwanaye.
Kanisa la Magharibi kwenye karne ya nne likahusisha hija ya mamajusi na toleo la Bwana jinsi ilivyo katika injili yetu ya leo. Mamajusi siyo Waisraeli hivyo wanawakilisha watu owte Mungu amejionyesha kwa watu wote hata sisi tuliopo hapa na kwa namna ya pekee leo kupitia hawa zetu. Tumshukuru Mungu hata leo anaendelee kujionyesha kwetu. Mamajusi waliona nyota ambayo kwayo Mungu aliwaelekeza kwenda kwa mtoto Yesu tunapenda kumwomba mwenyewzi Mungu ili ninyi muwe nyota ya kuwaongoza watu kufika kwa Mungu. Ninyi mue ile nyota ambapo watu watakapowaona katika maisha yenu ya kumcha Mungu waweze kutamani kumpenda na kumtumikia yeye zidi ya vitu vingine vyote na wawafuate kama mamajusi walivyofanya.

Maandiko ya Nabii Isaya 60, 1-6, yanadhihirisha wazi hilo watu kutoka sehemu mbalimbali wakiwa na vitu mbalimbali wakienda kumtukuza Mungu. Katika Isaya nusu mwanga utukufu wa Bwana wana na binti kutoka mbali utukufu wa habari na utajiri wa mataifa misafara ya ngamia na watu kutoka Medina wakichukua dhahabu ubani na manemane wakiutangaza ukuu wa Mungu. Hii ndiyo Epifania ya kweli.

Somo la pili toka barua kwa Efe. 3,2-3,5-6 linazungumzia juu ya ufunuo wa siri ya Mungu ambayo Mungu alidhamiria tangu awali. Ni mpango ambao makuhani wa kale waligusia lakini hawakujua maana kamili ya mpango huo. Mpango huo ulikamilika tu kwa njia ya Yesu kristo. Katika waraka kwa waefeso 1, 3-10, tunasoma juu ya wingi wa neema ya Mungu isiyopimika. Epifania ufunuo wa Mungu kwa njia ya Kristo ndiyo maana kamili ya maandiko matakatifu.

Somo la Injili tukumbuke kuwa ufunuo haukutokea kama hamu ya Mungu kujitosheleza bali kwa ajili yetu Mungu anapenda kuwa hata sisi tuuone utukufu huo hivyo tuinuke tumwelekee kama mamajusi walivyofanya. Yahitaji pia bidii yetu. Tujitoe sisi wenyewe kwake kama zawadi asante kwa ………. Zetu ambao wametambua upendo huo wa Mungu. Hakika hatuna budi kumshukuru Mungu siku hii ya leo pamoja na mtume Paulo kama anavyoandika katika waraka kwa wakolosai 1:3,12-20 twamshukuru Mungu baba yake Bwana wetu Yesu Kristo siku zote tukiwaombea mkishukuru Baba aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru…!

Matokeo ya ufunuo wake Bwana, tunawajibishwa ameweka wazi ushindi na utukufu wake mbele ya dunia yote. Tumshukuru Mungu hata leo anaendelea kujionyesha kwetu. Mamajusi waliona nyota ambayo kwayo Mungu aliwaekeleza kwenda kwa mtoto Yesu. Tunapenda kumwomba mwenyezi Mungu ili ninyi muwe nyota ya kuwaongoza watu kufika kwa Mungu. Ninyi muwe ile nyota ambapo watu watakapowaona katika maisha yenu ya kumcha Mungu waweze kutamani kumpenda na kumtumikia yeye zaidi ya vitu vingine vyote na wawafuate kama mamajusi walivyofanya.

1 Tim 6:14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

2 Tim 4, 1-8 kwa ufunuo wake kristo tunapata amri ya kuhubiri neno la Mungu ili upate taji la haki.

Tito 2,13 sisi tunatarajia baraka na mafunuo. Ebr 9:28 baada ya haya matarajio yetu ni kushiriki utukufu wa Mungu aliyejifunua kwetu.

Imetayarishwa na Pd. Reginald Mroso, C.PP.S.
Siku kuu ya Epifania Januari 6, 2015








All the contents on this site are copyrighted ©.