2014-12-31 10:24:20

Papa asikitishwa na mauaji ya Padre Gorostieta!


Baba Mtakatifu Francisko, amepokea kwa masikitiko makubwa habari za kifo cha Padre Gregorio Lòpez Gorostieta aliyeuwawa hivi karibuni huko Mexico. Katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu Maximino Martines Miranda, wa Jimbo Ciudad Altamirano, anapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa wote walioguswa na msiba huu wa kutisha na kwamba, anawakumbuka na kuwaombea katika sala zake.

Baba Mtakatifu anasema, haya ni mauji ya mtu asiyekuwa na hatia na wala hayana msingi wowote. Baba Mtakatifu anatumia fursa hii kulaani mauaji, nyanyaso na dhuluma dhidi ya utu na heshima ya binadamu. Baba Mtakatifu anawahamasisha Wamissionari Jimboni humo kusonga mbele kwa imani na matumaini bila kuogopa wala kukata tamaa licha ya magumu na changamoto wanazokabiliana nazo, huku wakifuata mfano wa Yesu Kristo mchungaji mwema. Baba Mtakatifu anapenda kuonesha mshikamano wake wa karibu kwa wazazi, ndugu na jamaa ya Marehemu Padre Gorostieta.







All the contents on this site are copyrighted ©.